Mkazi wa Kigugu kata ya Hembeti, Bakari
Kabua (54) akiuguza jeraha la kupigwa risasi eneo la mdomoni katika wodi
ya majeruhi ya wanaume hospitali teule ya wilaya ya Mvomero baada ya
kuzuka kwa vurugu zilizohusisha wakulima na wafugaji huku chanzo
kikidaiwa kuwa ni mmoja wa wafugaji kulisha mifugo katika shamaba la
wakulima katika mashamba
yaliyopo Mkindo
Novemba 4 mwaka huu na kupelekea watu zaidi ya wanne kupoteza maisha na
wengine 39 kujeruhiwa kwa risasi katika mapigano ya ana kwa ana mkoani
Morogoro.
Huyu ni mmoja wa kijana akiingizwa katika wodi ya wanaume ya hospitali hiyo baada ya kujeruhiwa kwa risasi.
Kundi la vijana wenye mishale na upindi wakiwa tayari kwa kujibu mashambulizi dhidi ya wafugaji, hapa ni kijiji cha Mkindo.
Nesi
wa Hospitali teule ya wilaya ya Mvomero Getruda Chambo kulia
akishirikiana na mwenzake kumhudumia mmoja kati ya 39 aliyepigwa risasi
baada ya kutokea vurugu za wakulima a wafugaji katika kata ya Hembeti
wilayai humo na kusababisha vifo vya zaidi ya mtu mmoja kufariki dunia
kwa kupigwa na risasi mkoani Morogoro. PICHA/MTANDA BLOG.
Post a Comment