Mgeni
Rasmi Mheshimiwa Mathias Chikawe akiongea na wajumbe wakati wa ufunguzi
semina ya wawakilishi na wabunge kuhusu masuala ya muungano.
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mada katika semina ya wawakilishi na wabunge kuhusu masuala ya muungano mjini Dodoma
Mmojawapo wa watoa mada Bwana Haule akiwasilisha mada katika semina hiyo mjini Dodoma.
Mmojawapo wa watoa mada Bwana Haule akiwasilisha mada katika semina hiyo mjini Dodoma.
…………………………………………………………………………….
Watanzania wameombwa kuwa
wavumilivu na watulivu katika muda huu ambapo mchakato wa katiba
unaendelea na kila mmoja ametakiwa kuweka mbele masahi ya taifa. Hayo
yamesemwa mjini Dodoma na Waziri wa Sheria na katiba Mheshimiwa Mathias
Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa semina ya wabunge na wawakilishi kuhusu masuala ya muungano .
Aliongeza kuwa watu wote watambue
kuwa katiba ni mali ya wananchi wote, ni dira ya wote na ni mwongozo
muhimu kwa taifa ili kuhakikisha linasonga mbele na kwa kuzingatia
misingi hiyo, ni wajibu wa kila mmoja kubaini kuwa hakuna aliye na haki
zaidi ya mwingine katika mchakato huu. Katiba bora ni ileinayotokana na
watu, inayoakisi matakwa ya watu na inayolenga kujenga na kustawisha
maisha ya watu wan chi husika alisema.
Akimkaribisha mgeni rasmi Waziri
wa Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu alisema Ofisi ya Makamu wa Rais
imeandaa semina hiyo ili kutoa uelewa wa masuaa mbalimbali ya muungano.
“Ofisi imeamua kufanya tathimini ya miaka hamsini ya utekelezaji wa
masuala ya muunganona kuweka muelekeo mzuri wa kushughulikia masuala
hayo” alisema
Katika ufunguzi huo pia
walikuwapo wataalamu mbalimbali ambao waliwasilisha mada zinazohusu
muungano kwa wajumbe wote wa semina hiyo. Na pia wajumbe walipata nafasi
ya kuuliza maswali na kuchangia
Post a Comment