Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mzee Moyo:amani iliopo Zanzibar imetokana na wazalendo

 

                           

Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo akiwahutubia maelfu ya wananchi katika mkutano mwa hadhara wa CUF Chaani
Wananchi wa Zanzibar wametakiwa kuelewa hali ya amani iliopo hivi sasa katika visiwa hii imetokana na mchango mkubwa wa viongozi wawili ambao ni wazalendo wa nchi hii akiwa ni Raisi mstaafu Mh,Amani karume pamoja na Maalim Seif.


Shauri hilko limetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo ambae pia aliwahi kuwa mwanasheria katika zama za mwanzo za utawala wa Mzee Karume katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Wananchi CUF uliofanyika Jimbo la Chaani hapo jana.

Mzee Moyo alisema Wazanzibar wanaposimama kudai urai wao pamoja na mambo mbali mbali ambayo yanaweza kuwaletea maendeleo ya hali ya juu katika nchi yao kuwa sio kosa kwani hapo awali Zanzibar iliweza kujiendesha wenyewe bila ya kuwepo kwa muungano.

Alisema kupitia mchakato wa katiba mpya ambayo wananchi wa Zanzibar wamedai mambo kadhaa yasiwe ya Muungano ambayo yatawawezesha Wazanzibar wenyewe kuwa huru kufanya wanachokitaka kwa maslahi ya Taifa lao,kufanya hivo sio kosa isipokuwa ni uhuru wa kila mwananchi kuamua anachokitaka kwa nchi yake.

Alieleza kazi kubwa ya kamati ya maridhiano Zanzibar ni kuhakikisha kuwa inaondosha chuki,ubaguzi na kila aina ya mfarakono. Ndani ya visiwa hivi ambapo kwa makusudi wamekuwa wakitokea baadhi ya watu kupandikiza chuki kwa wazanzibar.

‘’Tutahakikisha kuwa kila mzanzibar anaelewa lengo letu kwa nchi hii’’ alisema Mzee Moyo.

Maelfu ya wananchama wa Chama cha Wananchi CUF wakifuatilia kwa makini hutuba ya Mzee Moyo
Maelfu ya wananchama wa Chama cha Wananchi CUF wakifuatilia kwa makini hutuba ya Mzee Moyo,picha kwa hisani ya Hamed Mazrui 0774848800
Download Our App

1 comments:

Rais Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa Mhe James Mbatia

Reply

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top