Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali imeyataka makundi mbalimbali ya watu yanayopenda majina yao kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kufanya hivyo kabla ya Januari 2, 2014 saa tisa alasiri.


Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utaratibu wa kupata majina ya wajumbe watakaoteuliwa kwenye  Bunge la Katiba. Picha na Fidelis Felix.  
----
Serikali imeyataka makundi mbalimbali ya watu yanayopenda majina yao kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kufanya hivyo kabla ya Januari 2, 2014 saa tisa alasiri.

Pia imeyaagiza makundi hayo kuzingatia sifa zilizotajwa kwenye Sheria ya Marekebisho ya Katiba wakati wa uteuzi wa majina ya watu watakaowapendekeza.
             
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe alisema kuwa makundi hayo yanatakiwa kuwasilisha kwa Rais orodha ya majina ya watu wasiopungua wanne na wasiozidi tisa.

“Rais Jakaya Kikwete Desemba 13, 2013 alitoa tangazo kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2A) cha kifungu cha 22 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 alialika kila kundi kutoka pande zote za Muungano kuwasilisha kwake majina kwa ajili ya kuzingatiwa kwenye uteuzi,” alisema Chikawe.

Alibainisha kuwa kila kundi linatakiwa kuzingatia umri, jinsia, uzoefu, sifa na sehemu ya makazi ya mtu aliyependekezwa. Jumla ya idadi ya wajumbe kutoka Zanzibar hawatapungua moja ya tatu ya wajumbe wote.Kwa habari zaidi bofya na Endelea.......
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top