Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Abiria 48 wanusurika kufa baada ya basi la Shabiby kuanguka Singida.

Wakieleza kondakta wa basi hilo aina ya Yunton lenye usajili wa namba T 930 BUW ambaye amevunjika miguu yote miwili  bwana Thadei Muhando na mkaguzi wa basi la Shabubu bwana Williamu Ofyenge wamesema wakati basi lao lilikuwa liki lipita lori la mafuta gafla waliona basi lingine  liki wapita na kuwa magari matatu katika njia moja  na hatimaye dereva wao alishindwa kulimudu basi lao na kusababisha kupinduka.
Mganga mfawidhi wa  hospitali ya mkoa wa singida daktali banuba deogratius amethibitisha kupokea majeruhi  ishirini na nane ambao wanapatiwa matibabu na mgonjwa moja ambaye alikuwa kondakta wa basi amevunjika miguu yote miwili na wanampatia matibabu.
Kwa upande wake dereva wa roli la mafuta aina ya benzi lenye usajili wa namba raa 496n na tela lake lenye usajili wa namba rl 0255  ambalo lilikuwa likitokea nchi ya Rwanda bwana Hadimana Benjamini amesema alipitwa na mabasi mawili na moja  likamgonga upande wake na hatimaye kuanguka .
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi ambaye alifika katika ajali hiyo pamoja na kuwatembelea majeruhi amewataka madereva wote kuzingatia sheria za barabarani  ilikuweza kunusuru uhai wa watu na majeruhi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top