Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA),Dkt. Adelhelm
Meru, akimkabidhi zawadi maalumu mafanyakazi wa muda mrefu na mwenye
umri mkumbwa wa mamlaka hiyo, Bi. Easter Mkumbwa (kulia)kwenye hafla ya
kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 kwenye Hotel ya Land Mark
hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Wageni
waalikwa wakichukua chakula wakati wa hafla iliyo andaliwa na Mamlaka
ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA), ya kuuaga mwaka 2013 na
kuukaribisha mwaka 2014 kwenye Hotel ya Land Mark hivi karibuni jijini
Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA),Dkt. Adelhelm
Meru, akiwaongoza wafanyakazi na wageni waalikwa kulisakata Rhumba
kwenye hafla ya kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 kwenye
Hotel ya Land Mark hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Katika
kile kinachoonyesha kuzidi kufanikiwa kwa Tanzania katika nyanja ya
uwekezaji, Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA)
imetangaza kuvuka malengo yake kwa mwaka 2013.
Mafanikio
hayo yalitangazwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt.
Adelhelm Meru katika sherehe ya wafanyakazi ya kuuaga mwaka 2013 na
kuukaribisha 2014 jijini Dar es Salaam.
“Pamoja
na changamoto zilizopo hususani umeme, tunafurahi kuwa EPZA
tumefanikiwa na kuvuka malengo tuliyokuwa tumejiwekea mwaka 2013,”
alisema Dkt. Meru akiongea na waandishi wa habari.
Akiongelea
baadhi ya vigezo walivyotumia kujipima katika mafanikio hayo, Dkt. Meru
alisema mamlaka hiyo ilikuwa imejiwekea lengo la kupata wawekezaji
wakubwa 25 lakini kufikia mwishoni mwa mwaka jana walikuwa wamepata
wawekezaji 31 na hivyo kuvuka matarajio.
Pia
alisema pamoja na kujiwekea malengo ya kuvutia mtaji wa Dola za
Marekani 300 milioni kwa mwaka jana, mamlaka hiyo iliweza kuvuka lengo
na kuingiza nchini mtaji wa jumla ya dola za Marekani 498 milioni
nchini, ikiwa ni thamani ya fedha za wawekezaji walioingia nchini kwa
mwaka huo.
Mkurugenzi
huyo alisema EPZA ilikuwa imejiwekea lengo la kuzalisha ajira 5,200 kwa
mwaka jana lakini hadi kufikia mwezi Disemba jumla ya ajira 10,200
zilikuwa zimezalishwa kutokana na uwekezaji mpya uliofanywa kupitia
mamlaka hiyo.
“Tumevuka lengo hili kwa mara mbili na hii inatupa sana faraja kuwa kazi inafanyika,” alisema.
Akifafanua
zaidi alisema EPZA ilikuwa imejiwekea lengo la kuuza nje bidhaa zenye
thamani ya dola milioni 100 lakini lengo lilivukwa na kufikia dola
milioni 1005.
Alisema mafanikio hayo yote ni matokeo ya kufanya kazi kwa bidii na kuwashukuru wafanyakazi wote wa EPZA kwa juhudi hizo.
“Napenda kuwashukuru sana wafanyakazi wote wa mamlaka hii kwa mafanikio haya,” alisema.
Aliishukuru
serikali kwa msaada mkubwa inaoipa mamlaka hiyo katika kufanikisha
malengo yake hasa katika kupata wawekezaji na kutenga maeneo kwa ajili
ya uwekezaji na kuweka miundombinu muhimu inayotakiwa katika maeneo
hayo.
Alisema
malengo ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2014 ni kuvutia zaidi wawekezaji
katika maeneo maalum ya uwekezaji hapa nchini na hivyo kuendelea
kuimarisha uchumi wa nchi na kufikia maendeleo endelevu.






Post a Comment