Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
(kushoto) akimuongoza Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen (katikati)
alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam jana ili kujionea shughuli
mbalimbali za bandari hiyo kubwa kabisa Afrika Mashariki.
**********
Waziri Katainen alisema hayo wakati wa ziara yake aliyoifanya jana katika Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia ufanisi wake na kuendeleza uwekezaji wa Finland nchini.
Katika ziara hiyo, kiongozi huyo wa Finland aliambatana na maafisa wa serikali ya nchi yake, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Filberto Sebregondi, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Palangyo.
“Mkakati wa Rais wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now), huongeza kasi ya mchakato wa kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa ya kisasa zaidi. Wajibu wa sekta binafsi katika kufanikisha hili ni wa muhimu sana. Pia ninayo furaha kuona uwekezaji wa Finland kupitia kampuni zinazofanya kazi bandarini hapa,” alisema kiongozi huyo wa Finland.
Waziri Mkuu Katainen, pia aliipongeza jitihada zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha miundombinu ya bandari na usimamizi mzuri wa kuongeza ufanisi wa utoaji huduma bandarini hapo.
Kwa upande wake, Balozi Sebregondi, alisema, Umoja wa Ulaya umenuia kuwa mshiriki hai wa mazungumzo yanayohusu maendeleo ya biashara na sekta binafsi, ikiwa ni pamoja na mchakato huo wa kuifanya bandari hiyo kuwa ya kisasa zaidi, kati ya Mamlaka ya Bandari ya nchini (TPA) na umoja huo.
Ziara ya kiongozi huyo nchini ambayo ilimalizika jana, ililenga kudumisha uhusiano baina ya Tanzania na Finland na kuhamasisha maendeleo ya kibishara kati ya kampuni za kibiashara za mataifa hayo.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment