Mbunge Mgimwa ambae ameteuliwa kuwa naibu waziri wa maliasili na utalii akizungumza na wapiga kura wake jimboni
Mbunge wa Mufindi kaskazin Mahmood
Mgimwa kulia akiwa na mbunge wa Mufindi kusini Mendrady Kigolla na mkuu
wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu kushoto katika kikao cha uteuzi wa
wanafunzi wa waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka huu.(picha
na Francis Godwin Blog)
BAADA
ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri
ikiwa ni pamoja na kuteua sura mpya za mawaziri na manaibu kuingia
katika baraza hilo wananchi wa jimbo la Mufindi kaskazin
wamempongeza mbunge wao Mahmood
Hassan
Mgimwa kwa kuteuliwa kuwa naibu waziri wa maliasili na utalii na
kumwomba pindi atakapoapishwa kuanza kazi ya kufuatilia orodha ya
vibali vya vitalu vilivyotolewa na wizara ya maliasili na utalii ili
kuona kama haki imetendaka katika utoaji wa vibali hivyo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na mtandao huu wa www.matukiodaima.com katika
mahojiano maalum baada ya uteuzi huo leo walisema kuwa
wanampongeza Rais Kikwete kwa kumteua mbunge wao kuwa katika baraza
hilo na kutokana na mbunge huyo awali kabla ya nafasi hiyo kuonekana ni
mwenye shauku ya kusaidia wapiga kura wake katika maendeleo na kero
mbali mbali ikiwemo ya vibali ni wazi ataitumia nafasi hiyo kuweka
uwiano mzuri katika utoaji wa vibali vya vitalu katika msitu huo wa
Taifa wa Sao Hill Mufindi.
JOhn
Kalinga mkazi wa Mafinga alisema kuwa kilio
kikubwa cha wana Mufindi ni juu ya upendeleo ambao umekuwa
ukifanywa katika utoaji wa vibali ambapo baadhi ya watu wamekuwa
wakipewa vibali zaidi ya kimoja kwa kutumia majina tofauti jambo
ambalo linawanyima haki wasio na uwezo wa kufanya hivyo.
Kwani
alisema mbali ya kuwa mwaka huu vibali hivyo vimetolewa juzi ila
wapo baadhi ya watu wamepewa
kibali zaidi ya kimoja na kuwa suala hilo wanaomba Mgimwa kuweza
kufuatilia hasa ukizingatia msitu huo upo jimboni mwake kwa
asilimia kubwa zaidi na jimbo la Mufindi kusini kwa kiasi .
Hata
hivyo alisema imani ya wana Mufindi kwa baraza hilo ni kuona
linafanya kazi zaidi na wananchi ili kuweza kumsaidia Rais Kikwete
kumaliza muda
wake vizuri na CCM kuendelea kubaki madarakani .
Matrida
Sanga mkazi wa kinyanambo Mafinga alisema kuwa Rais Kikwete
hajakosea kumteua Mgimwa kuunda baraza la mawaziri kwani ni mmoja
kati ya wabunge wanaojituma sana katika kutumikia Taifa.
Japo
alisema imani ya wananchi wa Mufindi kwake ni kuona kero ya
wananchi wa mji wa Mafinga inayotokana na ucheleweshaji wa utoaji wa
vibali vya uvunaji mbao katika msitu wa Sao Hill na upendeleo
unakomeshwa ili kuepusha vijana kuingia mitaani kukaba watu kwa
kukosa ajira.
Katibu
mwenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi Daud Yassin
alisema kuwa wao kama chama wanampongeza Rais Kikwete kwa kumteua
mbunge wao kuingia katika baraza hilo kwa ni heshima kubwa katika
wilaya ya Mufindi ambayo imepata .
"
Kwanza utambue kuwa mimi ni katibu mwenezi wa CCM wilaya na Mgimwa
na
mbunge wangu kati ya wabunge wawili tulionao katika wilaya ya
Mufindi ....hivyo kuteuliwa kwake ni heshima kubwa katika chama na
kwa wakazi wa wilaya nzima ya Mufindi na mkoa wa Iringa"
Post a Comment