CHAMA Cha mapinduzi (CCM)
wilaya ya Iringa mjini kimesema kimejipanga kwa nguvu zote
kuhakikisha mbunge wa jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa anaachia jimbo
hilo hata kama hataki ikiwa ni pamoja na wiki tatu kwa mstahiki meya
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi kufuatilia kero
mbali mbali za wananchi ikiwa ni pamoja na kujua kiasi cha Tsh milioni
15 zinazotolewa kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya jimbo hilo kama
zinatumika vema .
Mbali ya hilo pia kufuatilia huduma
zinazotolewa katika vituo vya afya Hospital na Zahanati kama
zinafanyika kwa ubora ama zinafanyika kwa kuwanyanyasa wananchi.
"Ushindi
wa
Msigwa jimbo la Iringa mjini ulitokana na CCM wenyewe ila sasa
tunasema kamwe hatutarudia makosa yaliyojitokeza ni lazima turudishe
jimbo na Msigwa fedha zake azitumie vema asijaribu kuingia katika
ubunge tena"
katibu
wa CCM Iringa
mjini Hassan Mtenga aliyasema hayo juzi wakati wa mkutano wake wa
kwanza uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa toka alipohamishiwa
wilaya ya Iringa mjini akitokea Hai mkoani Kilimanjaro
Alisema zama za ubunge wa Mchungaji Msigwa katika jimbo la Iringa mjini umekwisha na sasa atake
ataondoka na asipotaka ataondoka.
"Mwambieni mbunge Msigwa wakati wa
kuwadanganya wananchi umekwisha na lazima sasa awaeleze wananchi wa
jimbo la Iringa mjini wapi anapelekea fedha za mfuko wa jimbo
ambazo zinatolewa kila mwezi na Rais Jakaya Kikwete"
Hata hivyo alimuagiza meya kupambana
ili fedha kiasi cha Tsh milioni 15 zinazotolewa na rais Kikwete kuona
zinafanya kazi gani katika ofisi ya mbunge pia kutembelea Hospital
na vituo vya afya ili kuona changamoto mbali mbali ndani ya wiki tatu
kupeleka majibu katika ofisi yake.
Kuhusu kupanda kwa gharama za umeme ni
matokeo ya Dr Slaa ambae alipigia kelele suala la Richmond na Dowans
ambapo baadhi ya wabunge waliunga mkono suala hilo ila leo baada ya
mambo kuwa magumu tunalalamikia suala hilo ambalo waasisi wake ni
Chadema kuleta kwele .
Alisema kuwa tunahitaji vijana
kuleta maendeleo ya mji wa Iringa na sio vijana wa kutumiwa kuvuruga
maendeleo ya mji wa Iringa.
" Nawaombeni wananchi kuwa tayari
tumemshika pua mbunge Msigwa na naomba wananchi tusaidiane kumnywesha
panado na ninamuomba Msigwa fedha za kiinua mgogo zake asije tena
katika jimbo la Iringa mjini atumie kwa kazi nyingine ....tumeanza
mkakati huu kwa ajili ya kumnyoa Msigwa "
Katika
mkutano huo wananchi walipewa nafasi ya kuwaweka kitimoto
madiwani wao ili kujibu kero mbali mbali za katani kwani huku
wananchi wa jimbo hilo la Iringa mjini wakikitaka chama hicho
kusaidia kukinusuru chama na kura za chuki kutokana na shirika la
ugavi wa umeme nchini (TANESCO) kuendelea kupandisha gharama za
umeme.
Wananchi hao walisema kuwa ili CCM jimbo hilo
na Tanzania kwa ujumla kiweze kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2015 na ule wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema
mwaka huu ni lazima gharama za umeme ishuke
Kwani
walisema kuwa hatua ya TANESCO kuendelea kuongeza bei ya umeme
ni kuongeza ugumu wa maisha kwa watanzania na kuwa ushindi wa CCM
utatokana na utetezi wa chama katika kuwaondolea mzigo wa bei ya
umeme watanzania.
Mbali
ya hilo pia wananchi wa kata ya Kihesa walimbana diwani wao Bw
Mussa Wanguvu kutokana na hatua ya kushindwa kupigania wananchi
ambao wanatakiwa kuvunja nyumba zao ambazo zimejengwa katika eneo
la Semtema Majengo mapya eneo ambalo halitakiwi kisheria
Diwani Wanguvu akijibu swali hilo alisema kuwa
eneo hilo lilizuiwa baada ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara hasa
wale ambao wamejenga katika mlima na wapo hatarini kuangukiwa na
mawe ila baadhi ya maeneo ambayo si rasmi ni waliachiwa .
Kwa
upande wao wananchi wa kata ya Mtwivila walimtaka diwani wao Bw
Victor Mushi kueleza ni lini atatekeleza ahadi yake ya zahanati na
ubovu wa barabara katika
eneo la Mkimbizi pamoja .
Kwa
upande wake diwani Mushi kuhusu suala la ujenzi wa kituo cha
afya alisema kuwa ahadi hiyo haikuwa ya kwake ila ilikuwa katika
ilani ya CCM japo alisema ujenzi wa mradi huo upo mbioni baada
ya kumaliza miradi ya zamani utaanza mradi huo wa ujenzi wa kituo
cha afya.
Kuhusu
barabara alisema kuwa kata hiyo wamejitahidi kutengeneza mifereji
na zaidi ya Tsh bilioni 1.8 zitatengeneza barabara ya lami kutoka
Mtwivila kwenda Mkwawa na tayari zoezi hilo linaendelea.
Katika
hatua nyingine
Mushi alipinga madai ya wananachi kuwa uongozi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa umekuwa ukifanya usafi katika mji kutokana na
kuwepo kwa ugeni ama vikao kuwa jambo hilo si kweli na kuwa
linafanyika kulingana na bajeti na ufinyu wake.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa
Ritta Kabati pia aliweza kueleza kazi mbali mbali alizozifanya katika jimbo la
Iringa mjini ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha polisi kwa gharama
zake eneo la Tumaini na kuwa ataendelea kuchonga sana juu ya kero
za wananchi wa Iringa mjini.
Kabati alisema kuwa kamwe hatarudi nyuma katika utendaji na kuwa
siku zote atawapigania wananchi wa jimbo la Iringa mjini na kuwa kuwa
siku zote kwake atahakikisha anatenda zaidi.
Akielezea mambo ambayo amepata
kutekeleza alisema ni pamoja na kusaidia sekta ya elimu vitabu na
kompyuta pamoja na kusaidia vikundi vya vikoba katika jimbo hilo la
Iringa mjini.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa
Aman Mwamwindi akijibu kero mbali mbali akianza na Hospital ya wilaya
ya Iringa mjini alisema kuwa Hospital hiyo imeendelea kutoa huduma .
Huku ujenzi wa barabara za lami
katika mji huo kupitia pesa za benk ya Dunia alisema barabara
itajengwa kuanzia Samora ,Hospital ya Frelimo , Itamba na maeneo
mengine ya mji .
Kuhusu suala la usafi alisema kuwa
moja kati ya sababu zilizopelekea mji wa Iringa kutoshika nafasi ya
kwanza ni kutokana na hadhi ya makaburi na ndio sababu makaburi ya
makanyangio kuanza kuzungushiwa uzio ili siku moja Manispaa ya
Iringa iweze kushika nafasi ya kwanza .
Alisema kuwa ni vema suala la
maendeleo ya mji wa Iringa lisifanyike kwa itikadi za vyama na
badala yake kufanyika kutokana na mazingira yaliyopo .
Kuhusu suala la Stendi ambalo
limeendelea kuleta lugha mbali mbali kutoka serikalini na viongozi wa
kisiasa alisema kuwa hashangai na kauli za upotoshwaji juu ya ujenzi
wa stendi hiyo ya kisasa ya mkoa itakayogharimu zaidi ya Tsh bilioni 4
fedha kutoka benki ya dunia .
Alisema kuwa mchakato wa ujenzi wa
stendi hiyo umeshirikisha wadau wote nyeti hadi mshauri wa mambo
ya kimazingira kimataifa na tayari ameifanya kazi hiyo na kutoa
maelekezo yake ya kitaalam ambapo ameruhusu ujenzi huo.
Alisema inapojengwa stendi hiyo kutoka
ukingo wa mto ni mita zaidi ya 700 wakati sheria ya ujenzi ya Rufiji na
Iruwasa ni mita kati ya 50 na 60 hivyo stendi hiyo ipo mbali zaidi
kuliko sheria.
Alisema kuwa fedha za ujenzi wa
stendi hiyo hata kama Halmashauri ingekusanya isingeweza kupata fedha
hizo ambazo hata kama ingekusanya kwa miaka zaidi ya 3 bila kupata .
Alisema kuwa wanaotumia maendeleo kwa
ajili ya kutafuta umaarufu katika siasa ni kutowatendea haki wananchi
ambao unawatumikia na kuwa suala la uongo halikubariki katika dini
zote .
Hata hivyo Mwamwindi alisema jitihada
mbali mbali zinazofanywa na serikali ya CCM katika manispaa ya
Iringa ni kutaka kuiwezesha Halmashauri hiyo kuja kuwa jiji kama
ilivyo Mbeya, Mwanza na Arusha .
Hivyo alisema tayari jitihada mbali
mbali za kuwezesha mji wa Iringa kuwa jiji na tayari wamepeleka
mradi wa maji Nduli mradi ambao wakati wa kuwekeana saini mbunge wa
jimbo la Iringa mjini alipata kushiriki .
"Tumepeleka barabara kutoka Tumaini
kwenda Kigonzile KM 6 tumepeleka mabati kwa ajili ya choo mgongo
pamoja na kuweka vituo katika eneo la Kigonzile ili kupeleka huduma
hiyo kwa wananchi ... kwa hiyo ndugu zangu mheshimiwa Mushi
amezungumzia barabara ya kutoka Mkimbizi hadi bima kiasi cha
mabilioni ya fedha ambazo binafsi sijapata kusaini fedha nyingi
kiasi hicho ....sasa tumeanzisha mkakati wa kugawa viwanja na
kupasua njia na ninasema kuwa ujenzi wa stendi upo pale pale na suala
hili lipo kwa waziri mkuu ambaye ndie mwenye TAMISEMI"
Wakati
huo huo katika mkutano huo CCM ilipokea wanachama zaidi ya 10
kutoka Chadema ambao walidai wameamua kurudi CCM baada ya kuona
Chadema kuna ubabaishaji mwingi. |
Post a Comment