Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KOCHA MPYA ALIYETUA NCHINI KUWASHAWISHI VIONGOZI WA YANGA KUMSAHAU MAXIMO


Kocha mpya wa Yanga aliyewasili nchini majuzi kwa ajili ya kuja kufanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo, Huns Plujim, akiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati alipokuwa akiwasili nchini. 

Wakati yimu ya Yanga ikiwa bado ziarani nchini Uturuki kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mechi za Kombe la Mataifa Afrika, anayetarajia kuwa kocha Mkuu wa timu hiyo amewasili nchi kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Klabu.

Taarifa za awali zilizokuwa si rasmi zilikuwa zikisema kuwa Klabu hiyo ilihitaji huduma ya aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars Mbrazil, Marxio Maximo, ambaye kwa sasa amelipotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa tayari imeshindikana kocha huyo kuja kukinoa kikosi cha Yanga kutokana na kutoelewana kwa upande wa malipo kwa dau alilohitaji la sh. milioni 26.

Aidha imeelezwa kuwa dau hilo ni pesa aliyoihitaji Maximo kama mshahara kwa mwezi, huku Maximo akiwa ni kati ya makocha 40 walioonyesha nia na kuomba kukinoa kikosi hicho ambapo pia alikuwa ni miongoni mwa makocha watatu waliobaki baada ya kuchujwa kutoka idadi hiyo kubwa.

Ikumbukwe Kocha huyo Maximo alipokuwa akiinoa timu ya Taifa Stars, alikuwa akilipwa kitita cha Sh. milioni 15 na Serikali, sasa kwa dau hilo alilolihitaji kutoka Yanga, Yanga itaipiku serikali kwa kukubali kumlipa dau hilo linalozidi dau alilokuwa akilipwa na Serikali au la. Tusubiri tuone mwisho wa mchezo ni nani atakabidhiwa Kikosi hicho cha watoto wa Jangwani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top