MTOA MADA: Niliwahi kutoa ahadi kuwa nitaweka sababu nzito Tano ambazo mimi binafsi naziona zinafaa sana kumtathmini Edward Lowasa kama Rais ambae Tanzania inamuhitaji kwa muongo mwingine ujao.
Nikiri wazi kwamba kwa CCM ni Lowasa pekee mwenye sifa hizo labda nitamlinganisha na Dr. Slaa ambae kwa muono wangu kidogo anamkaribia Lowassa nikimaanisha kidoogo wanalandana na nitasema wapi Lowassa anampiku Slaa.
Kwa
utangulizi tu ni kuwa Nchi hii ili iendelee inahitaji KIONGOZI kwa
ufupi kabisa niseme hivyo inahitaki KIONGOZI SHUPAVU tena SHUPAVU
KWELIKWELI sio masihara.
Waziri mkuu Mizengo Pinda na Mbunge wa Monduli Erdward Lowassa.
Tupo kwenye umaskini mkubwa,watu wanateseka bila sababu ya msingi. Vijana tunashabikia tuu kama wehu, wengine ni wasomi lakini tunapelekwa kama upepo tukisikia hiki "hewala" tukisikia kile "sawa" tukiambiwa hivi "alhamdulilah" tukiambiwa kile "poa tu".
Waziri mkuu Mizengo Pinda na Mbunge wa Monduli Erdward Lowassa.
Tupo kwenye umaskini mkubwa,watu wanateseka bila sababu ya msingi. Vijana tunashabikia tuu kama wehu, wengine ni wasomi lakini tunapelekwa kama upepo tukisikia hiki "hewala" tukisikia kile "sawa" tukiambiwa hivi "alhamdulilah" tukiambiwa kile "poa tu".
Hatutaki
kuchambua na kuielewa siasa kwamba kwenye siasa kuna majungu, fitna,
kuchongeana, uchu wamadaraka na mali na mambo meeeengi ambapo msipokua
makini mnaweza KUMCHUKIA MZURI MKAMPENDA MBAYA.
kwa misingi hii ninaanza uchambuzi wangu. Na uchambuzi huu nitauandika kwa facts and figures kamaanavyosemaga Prof.Muhongo.
1.LOWASSA NA "BIG RESULTS NOW".
Nianze
na hili.Tunajua wote kuwa serikali yetu sasa ipo kwenye mpango wa
matokeo makubwa sasa BRN. Mpango huu mbali na mambo mengine unahitaji
kiranja mkuu (RAIS) ambae ni SHUPAVU,JASIRI, MTHUBUTU,MWENYE KUWEKA
MALENGO NA KUSIMAMIA KUONA YANATEKELEZEKA lakini pia kama jina la mpango
lenyewe lilivyo "MATOKEO MAKUBWA SASA" yaani we want things to happen
now.
Kwa minajili hiyo ni kiongozi gani mnaeona anaeweza kuleta matokeo makubwa sasa?embu tuwe wakweliLOWASSA tunamjua alipoingia kuwa waziri mkuu alitangaza kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ambacho angekuwa WAZIRI MKUU angetaka kata zote ziwe na shule za sekondari. Sote ni mashahidi alivyosimamia sera hiyo shule zilianza kumea kama uyoga yaani kama mazingaombwe.
Hata maeneo kama ya Kinondoni ambapo ardhi huuzwa kiholela hivyo ardhi kutopatikana lakini ilipatikana kuanzia vijijini hata miji wananchi walianza kujenga shule.ni mashahidi kama sio fitna za yeye kupelekea kujiuzulu sijui leo kielimu tungekuwa wapi.
HE HAD A MASTER PLAN OF OUR EDUCATION SYSTEM AND HE LEFT WITH IT BUT STILL HE HAS IT IN HIS HEAD.
Naamini
huyu mzee akipata nafasi tutafika. Si hilo tu tunajua mambo mengi
aliyokuwa nayo kichwani ambayo mengi yapo kwenye huu mpango ni shupavu
ambae angeweza na anaweza kuyasimamia yatekelezeke. Dr.Slaa ni mzuri wa
kusimamia mabo lakini somtimes huwa analoose focus nitaliongelea kwenye
point ya tatu.
2.LOWASSA ANAJUA KUWEKA VIPAUMBELE NA KUJUA TUNAVIFIKIAJE.
2.LOWASSA ANAJUA KUWEKA VIPAUMBELE NA KUJUA TUNAVIFIKIAJE.
Jamani
Nchi hii ili iendelee na ndivyo hata nchi zilizoendelea zilivyoanza ni
kuwekeza katika elimu ya watu wake, Kilimo na Viwanda nikimaanisha sekta
ya uzalishaji. Tunajua jinsi LOWASSA alivyo anza na hayo shule za kata
nilishazizungumzia na mipango mingi ya elimu ukitaka kuijua waulize
walimu alipoanzisha program ya kuwajengea nyumba,alivyoanzisha program
ya kuhakikisha watoto hawakai chini kila mtoto akae kwenye
dawati,alivyoshusha ada n.k
Tusisahau
kwenye kilimo aliyoanzissha kilimo cha umwagiliaji mpaka akataka kuleta
Mvua ya kutengenezawa mimi huwa nasema hata kama isingewezekana lakini
inaonyesha ile nia njema aliyonayo mzee huyu.
Ukitaka kuelewa vizuri waulize wakulima wakuhadithie jinsi alivyokua anawatimua kazi na kuwashtaki watu waliokua wanakula hela za mbolea za ruzuku. Jinsi alivyokua anatafuta masoko ya nje ya mazao ya kilimo waulize wafanyabiashara wakuhadithie.
Ni kiongozi nani mwenye hulka na kariba hii ndani ya CCM? Tunajua wote kuwa mapinduzi ya kilimo na viwanda ndiyo yaliendeleza bara la ulaya historia inatuambia hivyo na elimu ndiyo imeikomboa JAPAN na nchi nyingine LOWASSA ni jenmbe katika hili ana master plan ya mambo haya na anajua kusimamia haya sio siri wala kumpigia debe HE IS REAL.
3.LOWASSA SIO MTU WA KUPOTEZA UELEKEO (TO LOOSE FOCUS)
Lowassa siku zote akitaka kitu ni mpaka kitimie na kikishindikana basi ujue kumpata wa kukiweza ni shughuli pevu na akitaka kitu hakati tamaa idimradi kiwe ni chema hata kama hakina maslahi kwake na ikitokea yeyote akasimama mbele yake kumzuia basi ama zake ama za huyo mtu. wazungu wanasema "You are either with me or against me".
Tunakumbuka jinzi alivyokua akitimua viongozi waliokuwa wakitaka kumkwamisha kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Hakujali urafiki wala nini anakuweka ukimzingua anakumwaga THAT IS THE TYPE OF THE PRESIDENT WE WANT kwa sifa hii hana tofauti na Dr. Slaa japo Slaa huwa wakati mwingine anapoteza uelekeo.
Mfano mzuri wa kutopoteza uelekeo ni kwamba mwaka 1995 alitaka kuwa Rais wakatoswa,2005 akakubali swahiba wake achukue lakini akabaki kuwa focused, fitna zikajengwa akajiuzulu 2007 lakini hata sasa bado hajaloose focus japo anaface a lot of challenges.
Sio mfano mzuri sana huo kutoa lakini inaonyesha ni mtu wa namna gani kuwa siku akitaka vijana tukimaliza vyuo tupate kazi maana yake atalisimamia hilo by hooks or crooks kama ni viwanda kufufuliwa vitafufuliwa idimradi tu vijana tulambe ajira THAT IS THE PRESIDENT WE WANT. A FOCUSED MAN
4.LOWASSA NI HALF DICTATOR HALF DIPLOMATIC
Hahahahaha nianze kwa kucheka maana tunajua hakuna nchi iliyoendelea kwa kiongozi kuwa full diplomatic yaani kitu kidogo "Tume iundwe" jambo dogo "NJOO MEZANI TUONGEE" kitu kidogo "TUSUBIRI UCHUNGUZI" jambo kidogo "DUNIA ITATUELEWAJE". jamani tunamjua.
Lowassa
ni mtu wa action kwa kwenda mbele Ghorofa limeanguka nani mkandarasi
piga chini. Halmashauri imekula hela za maendeleo nani mkurugenzi piga
chini. Wizara inatokota nani muhusika piga chini. Tunatatizo fulani
solution ni nn tekeleza.yaani hakuna longolongo.Hii ndio type ya uongozi
itakayotukomboa Tanzania.
Na
ukitaka kujua faida yake waulize wachina yaani watakwambia vizuri
udictator kidogo unavyoharakisha maendeleo yao. Hakuna TANZANIA hii
viongozi wa type hii mbali na LOWASSA na Dr. SLAA tatizo SLAA
....(nitamuongelea wakati mwingine)
5.LOWASSA ANASIKILIZIKA, ANAFUATILIA, SI KIGEUGEU NA SI MVIVU.
5.LOWASSA ANASIKILIZIKA, ANAFUATILIA, SI KIGEUGEU NA SI MVIVU.
Hii
ni sifa kubwa kwa mtu kuwa RAIS unapoona unataka kuwa Rais au
unamchagua mtu ambae kwa haiba yake tu hasikiliziki ujue unaturudisha
nyuma.
Rais
anatakiwa awe akisema hili lifanyike huyo anaeambiwa linamuingia
moyoni. Nirudie Rais anatakiwa anapoongea hata kwa simu tu ile pitch ya
sauti iashirie kuwa jambo hili ni lazima lifanyike.Yaani kama anaongea
mbele yako ukimwangalia kuanzia nywele mpaka unyayo uashirie kuwa
kiongozi anataka hili lifanyike.
LOWASSA yupo hivyo akisema jambo linatekelezwa na haiishi hapo anafatilia mwanzo mwisho si mvivu hata kidogo.kutwa anaizunguka Tanzania hii vijijini hadi mijini nyote ni mashahidi wa hili.
LOWASSA yupo hivyo akisema jambo linatekelezwa na haiishi hapo anafatilia mwanzo mwisho si mvivu hata kidogo.kutwa anaizunguka Tanzania hii vijijini hadi mijini nyote ni mashahidi wa hili.
Post a Comment