Katibu
Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutubia wafuasi na
wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni za udiwani uliofanyika
kata ya Magomeni Wilayani Bagamoyo.
Katibu
Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akimnadi mgombea udiwani kata
ya Magomeni, Njema Seif Mohd, katika mkutano wa kampeni za udiwani
uliofanyika kata ya Magomeni Wilayani Bagamoyo
Naibu
Katibu Mkuu wa CUF (Bara) Julius Mtatiro akiwahutubia wafuasi na
wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni za udiwani uliofanyika
kata ya Magomeni Wilayani Bagamoyo.
Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari na Uenezi (CUF) Abdul Kambaya, akizungumza na wafuasi na wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni za udiwani uliofanyika kata ya Magomeni Wilayani Bagamoyo.
Baadhi
ya wakaazi wa kata ya Magomeni Wilayani Bagamoyo wakisikiliza kampeni
za CUF zilizozinduliwa na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad. (picha
na Salmin Said, OMKR)
Na Hasssan hamad , OMKR
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amefungua
kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Magomeni Wilaya ya
Bagamoyo, na kuwanasihi wakaazi hao kutochagua viongozi wanaojihusisha
na vitendo vya rushwa.
Amesema
kiongozi atakayechaguliwa kwa kutoa rushwa, kamwe hatoweza kukemea
vitendo hivyo na badala yake ataviendeleza na kuwaacha wananchi
wakibakia katika hali ya umaskini na matatizo mengi katika maeneo yao.
Maalim Seif amewashauri wakaazi hao kusikiliza sera za wagombea
wote, ili waweze kuzipima na kuzichambua na hatimaye kuchagua kiongozi
atakayewajali na kusaidia kuwatatulia kero zinazowakabili.
Amesema
mgombea wa CUF katika kata hiyo nd. Njema Seif Mohd, ameonesha dalili
njema kwa kuwa mwaminifu na mtu anayewajali wenzake, na kuwataka wakaazi
hao kutofanya makosa katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe
09 mwezi ujao.
Kwa
upande wake, mgombea wa udiwani CUF katika kata hiyo ya Magomeni
Wilayani Bagamoyo nd. Njema Seif Mohd ameahidi kusimamia matatizo
yanayowakabili wakaazi hao kwa lengo ya kuyatafutia ufumbuzi.
Akitaja
vipaumbele vyake amesema atasimamia suala la elimu ili kuhakikisha kuwa
watoto wote wanakwenda skuli bila ya vikwazo vyovyote, pamoja na
kusimamia upatikanaji wa vifaa vya hospitali ikiwa ni pamoja na madawa.
Aidha amesema atasimamia mapato ya halmashauri hiyo ili kuona kuwa yanatumika kama yalivyokusudiwa.
“Nichagueni tutetee Magomeni yetu”, alijinadi Njema.
Mapema
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara Julius Mtatiro, alishutumua
utendaji wa halmashauri hiyo na kudai kuwepo kwa matumizi mabaya ya
fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Post a Comment