Ferouz (mwenye kofia) akiwa chini ya ulinzi

Kila kukicha kuna wasanii wa maigizo na filamu ambao tunasikia
wamekamatwa na madawa ya kulevya, "unga" katika jitihada za 'kusaka
maisha', wenyewe wanasema kuna ajali kazini. Wasanii hao ambao wengi ni
vijana, na pale wanapoonekana kwenye runinga huwa hamasa kwa wadogo zao
na jamii kwa ujumla, wakipenda kuwa kama wao.
Na mchana huu, maeneo ya Sinza, kuna taarifa ya mwanamuziki aliyetamba
kwenye muziki wa bongo fleva, Ferouz, sanasana kwa wimbo wake wa
Starehe, ambao ulikuwa ukionyesha madhara ya UKIMWI na virusi vya
UKIMWI. Ferouz anadaiwa kukutwa na bangi, na picha ambazo Gospel Kitaa
imezipata eneo la tukio, zinamuonyesha akisindikizwa na maafande kunako
mbele ya vyombo husika.
Vijana wa Tanzania tuna shida
gani? Kama ni ardhi tunayo, kama ni nguvu tunazo, sasa nini shida zaidi?
Ipo haja ya Operesheni ambazo Askofu Sylvester Gamanywa ameitisha za
Takasika iliyomalizika hivi karibuni, na kisha kupokelewa na Operesheni Milikisha,
kuwahusisha pia wasanii wa aina zote, maana wanaonekana kukumbwa na
janga hili kwa sana, vinginevyo, vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa
watakuwa wakijaa jela za ndani na nje, wakiacha wageni kuja kutawala.
on Tuesday, January 14, 2014
Post a Comment