*********
Marekani. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyanzo vya ndani vya
Ikulu ya Marekani, wenza hao wamekuwa katika migogoro na Obama
alilazimika kusherehekea sherehe za mwaka mpya mjini Hawaii akiwa na
binti zake wawili, Sasha na Malia bila kuwepo Michelle.
Jarida la National Enquirer lilieleza kwamba
katika moja ya matukio, Obama aliwahi kukutwa akiwa na mwanamke mwingine
katika ‘mazingira ya kutatanisha’ wakati mkewe akiwa safarini.
Kutokana na ripoti iliyotolewa na Bombshel ,
Michelle na Obama wamekuwa wakilala vyumba tofauti ndani ya Ikulu.
Michelle pia anajiandaa kuhama katika jumba lao pale Chicago ambalo
wameishi wakati wa uchumba wao miaka 21 iliyopita na kwa msisitizo
watajadili juu ya talaka.
Taarifa ilidai tatizo limeanza miaka minane
iliyopita pale Obama alipodhamiria kujijenga kisasa. Ni mtoto wao Sasha
ambaye aliumwa ugonjwa unaosababishwa na woga wa maisha unaoitwa Spinal
Meningitis ndiyo uliowafanya waendelee kuwa pamoja.
Kitabu cha Anderson kinaelezea tatizo lilivyoanza
baada ya Barack Obama kuamua kuingia kwenye siasa, ambapo Michelle
alisikika akimwambia mumewe; “Wewe unajifikiria mwenyewe tu.”
Naye Barack Obama amesikika akisema: “Sikuwahi
kufikiri kamwe kwamba ningelea familia mwenyewe siku moja.” Anderson
anadai kuwa Obama amechoshwa na malalamishi ya mkewe.
“Nampenda sana Michelle lakini ananiumiza na
ubishi wake wa kila mara,” alisikika akisema Obama na kuongeza kuwa;
“Anaonekana ni mwingi wa machungu na hasira siku zote.”
Akizungumza na televisheni ya CBS ya Marekani,
Anderson alidai kuwa ilikuwa nusura Michelle atembee nje ya ndoa kwa
sababu ya upweke.
Kwa miaka mitano wamekuwa na wasiwasi juu ya uwezo
wao wa kupata watoto kabla Malia hajazaliwa. Walishajadili sana suala
la kuasilia watoto (adoption) na marafiki zake wa karibu lakini kwa
bahati nzuri Malia alizaliwa mwaka 1998 na kuondoa wazo hilo.
Jina kamili la Obama ni Barack “Barry” Hussein
Obama, Jr, alizaliwa Agosti 4, 1961 Honolulu, Hawaii, alikulia huko huko
Hawaii na Indonesia, baba yake mzazi ana asili ya Kenya. Jina kamili la
mkewe ni Michelle LaVaughn Robinson, alizaliwa Januari 17, 1964
Chicago, Illinois.
Kukutana kwako
Barack na Michelle walikutana mwaka 1989 katika
mazingira ya kikazi, walifunga ndoa Oktoba 18, 1992, katika Kanisa la
Umoja wa Kristu la Trinity lililopo Chicago, Illinois
MWANANCHI
Post a Comment