Wakufunzi
wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Katibu Tawala Msaidizi wa
Mkoa sekta ya Elimu Wariambora Nkya (hayupo kwenye picha) aliyefunga
mafunzo ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014 kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendela
Katibu
Tawala Msaidizi wa Mkoa sekta ya Elimu, Wariambora Nkya, (wapili kutoka
kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya
wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014,
mara baada ya kufunga mafunzi hayo, jana kwenye ukumbi wa Edema, Mjini
Morogoro ( wapili kutoka kushoto) ni Mkurugenzi wa Sensa ya watu na
Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo.
( Picha zote na John Nditi).
……………………………………………………………
(Na Veronica kazimoto – Morogoro)
19 Januari, 2014.
Viongozi
wote wa Serikali katika ngazi zote kwa ujumla wameombwa kutoa
ushirikiano katika kuhamasisha na kuelimisha umma umuhimu wa
kushirikiana na Wadadisi pamoja na Wasimamizi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi unaotarajia kuanza rasmi mwezi Februari na kumalizika Disemba mwaka 2014.
Hayo
yamesemwa jana na Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Morogoro Wariambora
Nkya wakati akifunga Mafunzo ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye
Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Edema mkoani Morogoro.
Nkya
amefafanua kuwa ni muhimu viongozi wote wa Serikali kutoa ushirikiano
kwa wadadisi na wasimamizi kwani utafiti huo ni muhimu katika kuboresha
sera na program mbalimbali za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia
utekelezaji wa mipango ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira
ya Maendeleo ya mwaka 2015 na Malengo ya MKUKUTA na MKUZA.
“Nitoe
wito kwa viongozi wote wa Serikali kutoa ushirikiano kwa Wadadisi na
Wasimamizi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014
ili waweze kutekeleza majukumu yao kama ilivyopangwa”, amesema Nkya.
Wakati
huo huo Katibu Tawala Nkya amewaomba Wananchi kutoa ushirikiano wa
kujibu maswali na kutoa taarifa sahihi wakati watafiti watakapopita
katika makazi yao kukusanya taarifa za soko la ajira katika ngazi ya
Kaya.
“Napenda
kuwahakikishia Wananchi kwamba shughuli zao za kiuchumi na kijamii
hazitasimamishwa na zoezi la Utafiti huu kwa kuwa Wadadisi watakusanya
takwimu za Utafiti huu wakati shughuli zingine zikiedelea kama
kawaida”, amesisitiza Nkya.
Wariambora
Nkya ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera
na mafunzo hayo ya wiki mbili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu yamemalizika ambapo jumla ya Wakufunzi 60 kutoka mikoa
mbalimbali nchini walihudhulia mafunzo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Katibu tawala msaidizi wa mwaka 2014 huu katika maeneo yatakayohusika.
Ukosefu
wa Ajira umekuwa ni changamoto kubwa kwa sasa duniani kote ambapo
ripoti ya mwaka 2013 ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu hali ya
ajira duniani, inaonesha kuwa takribani watu milioni 197 sawa na
asilimia 5.9 ya nguvu kazi duniani hawana kazi.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Dkt. Milton Mahanga
wakati akifungua Mafunzo ya Wakufunzi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa
Kufanya Kazi wa mwaka 2014 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Edema
uliopo Morogoro mjini.
Dkt.
Mahanga amesema kati ya watu 197 ambao hawana kazi vijana ni milioni
73.8 sawa asilimia 12.6 ambayo ni nguvukazi inayopaswa kutumika ipasavyo
kwa kuwa kuna mahusiano makubwa kati ya ukuaji wa tija na matumizi ya
nguvukazi.
Ameongeza
kuwa, kutokana na changamoto hiyo ya ajira, ni muhimu kufanya Utafiti
wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya kazi ili kuisaidia Serikali kufuatilia
mwenendo wa mabadiliko yanayotokea katika soko la ajira.
Mahanga
amefafanua kuwa utafiti huu utasaidia pia kuboresha sera na program
mbalimbali za kukuza ajira, kupanga na kufuatilia utekelezaji wa mipango
ya maendeleo kama vile Malengo ya Milenia, Dira ya Maendeleo ya mwaka
2015 na Malengo ya MKUKUTA na MKUZA.
Kwa
upande wa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Ephraim Kwesigabo amesema lengo kuu la Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa
Kufanya Kazi ni kukusanya takwimu zinazohusu hali ya soko la ajira
nchini.
Kwesigabo
amesisitiza kuwa utafiti huo utawezesha kupata viashiria vinavyohusu
ajira na ukosefu wa ajira kwa makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii
na hivyo kuisaidia Serikali kuboresha sera ya kukuza ajira nchini.
Mafunzo
hayo ya wiki mbili yameandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambapo
jumla ya Wakufunzi 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaendelea kupewa
mafunzo juu ya Utafiti huo wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi
utakaoanza rasmi mwezi Februari hadi Disemba mwaka 2014.
Post a Comment