Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Pinda aenda Kiteto leo

Waziri Mkuu Pinda akishuka kwenye ndege

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo anakwenda Wilaya ya Kiteto, Arusha kutafuta suluhu ya mapigano baina ya wakulima na wafugaji katika Hifadhi ya Embroi Murtangosi yaliyosababisha vifo vya watu 10.

Mwandishi wa Habari wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Irene Bwire alisema jana: “Ni kweli Waziri Mkuu atakwenda kutembelea wilayani Kiteto ili kuongoza juhudi za kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.”



Polisi waanzisha msako

Maofisa wa Polisi kutoka Makao Makuu ya jeshi hilo wanaongoza operesheni ya kuwasaka wahusika wa mapigano hayo kwa kutumia helikopta.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alisema msako huo unaongozwa na Kamishna wa Operesheni wa Polisi, Simon Sirro... “Operesheni inaendelea porini lakini hadi sasa hatujakamata mtu. Mapigano yanayoendelea Kiteto ni ya kuviziana.”

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Martha Umbulla amezitaka pande zote kuacha vita na kuwataka waliovamia ardhi ya Kiteto kuondoka kwa hiari.

Chadema waibana Serikali

Waziri Kivuli wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Rose Kamili ameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kumaliza mgogoro huo.

Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Kamili alisema licha ya Bunge kuunda kamati kwa ajili ya kuchunguza migogoro ya wakulima na wafugaji nchi nzima, hali bado ni tete katika eneo hilo.

Alisema Serikali inatakiwa kujitafakari juu ya uwezo wake wa kushughulikia matatizo ya haraka, badala ya kuwa mabingwa wa kushughulika na matokeo ya tatizo.

Mgogoro

Mgogoro huo ulioanza mwaka 2006, unatokana na wafugaji na wakulima kugombea ardhi kwenye eneo la Hifadhi ya Embroi Murtangosi.

MWANANCHI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top