Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi, Meya wa Jiji
la Dar es Salaam, Didas Masaburi kutokana na kifo cha Diwani wa Kata ya
Mchafukoge, Jijini Dar es Salaam na mbunge wa zamani wa Dodoma Mjini,
Hashim Sagaf. Katika salaamu hizo, Rais Kikwete alisema kuwa
amesikitishwa na kuhuzunishwa na kifo cha Sagaf, kilitokea juzi katika
Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam na kuzikwa jana mjini Dar es
Salaam.
“Nimepokea kwa huzuni na masikitiko taarifa za
kifo cha Sagaf. Nilimfahamu Sagaf kwa miaka mingi. Alikuwa ni kiongozi
hodari wa umma. Alikuwa raia mwaminifu kwa nchi yake na mzalendo wa
kweli.”
“Nakutumia wewe Mheshimiwa Masaburi, Meya wa Jiji
la Dar es Salaam, salamu za dhati ya moyo wangu za rambirambi kuomboleza
kifo cha Sagaf. Aidha, kupitia kwako, naomba uniwasilishie salamu zangu
za pole nyingi kwa ndugu, jamaa na wanafamilia za Mheshimiwa Sagaf,”
alisema Rais Kikwete katika rambirambi zake.
Katika hatua nyingine, Tanzania imefanya vizuri na
kuonyesha mafanikio kuliko nchi nyingine yoyote duniani kati ya nchi
nane zilikuwa zinashiriki Mpango wa Majaribio wa Kuuwezesha Mfumo wa
Umoja wa Mataifa Kufanya Kazi kwa Pamoja.
MWANANCHI
MWANANCHI


Post a Comment