Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Simba uso kwa uso na Mtibwa Sugar Jumamosi

 


 

imagesMABINGWA wa Mtani Jembe na washindi wa pili wa michuano ya Mapinduzi, Jumamosi watajitupa katika Uwanja wa Taifa, kuvaana

na timu ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo wa kirafiki utakuwa wa mwisho kwa klabu ya Simba,

kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, inayoanza kutimua

vumbi Januari 25 mwaka huu.


Akizungumza Dar es Salaam jana Kocha msaidizi wa Simba,

Suleiman Matola, alisema wameamua kupata mechi moja katika

uwanja wa taifa kabla ya kuanza kwa ligi.

Matola alisema sababu kuu ya kuamua kucheza mchezo huo ni

moja ya sehemu yao ya kuipa timu yao mazoezi katika uwanja wa

Taifa, ambao itachezea mechi zake za nyumbani.

Alisema wameamua kucheza mechi na timu ya Mtibwa, kwa

sababu wanaitambua bora wake, hivyo wakicheza nayo inawapa

maandalizi mazuri.

Matola alisema kuwa mchezo huo utafanyika majira ya saa 10.jioni,

ikiwa ni moja ya sehemu ya kocha wao Zdravko Lugarusic, kutaka

timu ngumu, ya kucheza na timu ya Simba.

“Haya ni maamuzi ya kocha mkuu Logarusic, anataka kuichezesha

timu yake na timu ngumu, ambayo itaipa mazoezi mazuri timu

yake, kabla ya kuanza kwaa ligi kuu”alisema Matola.

Simba iliyorejea juzi jijini Dar es Salaam, ikirtokea Zanzibar katika

michuano ya Mapinduzi, ambapo ilifika hatua ya fainali na kupata

ushindi wa pili wa michuano hiyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top