Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Taarifa kuhusu kujiunga na JKT kwa hiyari/kujitolea 2014

 



Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) litaandiksiha vijana wa kujiunga na JKT kwa kujitolea kuanzia Januari 2014.


Nafasi hizo zimetolewa kwa Tanzania Bara na Visiwani.

Usaili utaanzia ngazi za Wialaya hadi Mkoa. Vijana wanaopenda kujiunga na JKT kwa kujitolea kwa kipindi cha miaka miwili wapelekea maombi yao kwenye Wilaya waliko.

Mafunzo yataanza mwezi Machi kwa watakaochaguliwa.

Sifa na masharati kwa
mwombaji:-



  1. Awe raia wa Tanzania.

  2. Awe na umri wa miaka 18 hadi 23.

  3. Awe na elimu ya darasa la saba hadi kidato cha sita.

  4. Asiwe ameoa, kuolewa na asiwe na mtu anayemtegemea.

  5. Awe tayari kurudi nyumbani baada ya kumaliza mkataba wake na Jeshi la Kujenga Taifa.

  6. Awe na tabia na mwenendo mzuri.

  7. Awe tayari kufuata sheria zote  za Kijeshi zitakazokuwa juu yake wakati akiwa Jeshini (kutoroka, wizi, ulevi, uvutaji bangi, madawa ya kulevya , upatikanaji wa mimba n,k) Jeshini ni makosa makubwa na utaweza kushitakiwa na kusitishiwa mkataba wako na Jeshi la Kujenga Taifa.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top