Baadhi
ya wakazi wa kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa
Singida, wakitoa miili ya abiria wa Noah T.730 BUX waliofariki baada ya
gari hilo kugongwa na lori aina ya Scania T.687 AXB kwenye barabara kuu
ya Singida – Dodoma leo. Noah hiyo ilikuwa ikitoea Itigi wilayani
Manyoni akienda Singida mjini.(Picha na Nathaniel Limu).
Gari aina ya Noah T,730 BUX linavyoonekana baada ya kugongwa na Lori.
Gari aina ya Noah T,730 BUX linavyoonekana baada ya kugongwa na Lori.
ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa
familia moja wamefariki dunia mkoani Singida leo, baada ya gari
walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK, kugongwa na Lori aina ya
Scania.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya miili ya abiria wa Noah T,730
BUX waliofariki leo kwenye ajali iliyotokea eneo la kijiji cha Isuna
tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi baada ya kugongwa na lori T.687
AXB.(Picha na Nathaniel Limu).
Ajali hiyo ya kusikitisha
imetokea leo saa 1.32 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo
la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa
likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya kuja Singida
mjini.
Amesema hadi sasa miili ya
abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria
watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye chumba
cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida
Alitaja waliotambuliwa na
makazi yao kwenye mabano kuwa ni Omari Shaban (44) na mke wake Salma
Omari na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi mjini.
Kamwela alitaja wengine kuwa
ni Haji Mohammed (29) (Msisi),Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda),Salehe
Hamisi (28) (Sajanranda),Samir Shaban (20) (Puma),Mwaleki Nkuwi (35)
(Ikungi),Athumani Kalemba (38) na Ramadhan Mkenga (Sajaranda).Katika
ajali hiyo,abiria watatu walinusurika na kupata majeraha madogo madogo.
Amefafanua juu ya ajali
hiyo,Kamanda huyo alisema kuwa lori aina ya scania T.687 AXB wakati
likipishana na noah,lilihama upande wake na kuifuata noah ambayo ilikuwa
upande wake wa kushoto,na kuligonga na kisha kuliburuza kati zaidi ya
15.
“Kwa sasa bado hatujajua
chanzo cha ajali hiyo mbaya ingawa baadhi ya watu wanadai kuwa huenda
dereva wa lori alisisia na kusababisha lori hilo kuhama upande wake na
kufuata noah.Uchuguzi utakapokamilika,tutatoa taarifa hiyo”,amesema.
Wakati huo huo,mganga mfawidhi
wa hospitali ya mkoa mjini Singida,Dk.Banuba Deogratius amekiri kupokea
miili ya abiria hao 13 na kusema kati yao,watoto ni
wawili. http://dewjiblog.com





Post a Comment