Ikumbukwe mawaziri waliotajwa kuwa ni mizigo ni pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza na Naibu wake, Adam Malima kuwa wameshindwa kazi na kupendekeza wang’olewe.
Kauli hiyo ambayo ilitolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, akisema kuwa mawaziri hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia Watanzania.
Alisema anasikitishwa na kitendo cha mawaziri hao waliopewa dhamana kushindwa kutambua wajibu wao na kwamba umefika wakati wa kuhojiwa na Kamati Kuu (CC) ya CCM ili wachukuliwe hatua kwani bila kufanya hivyo aibu itarudi kwa chama chake.
Nape alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wakati akielezea changamoto zinazowakabili wakulima ambao ni asilimia 80 ya Watanzania, huku mawaziri husika wakikaa kimya.
Alisema kuwa Waziri Chiza na Malima wamebaki wakifunga tai na kuvaa suti mjini wakati wakulima wa Ruvuma na mikoa mingine ya Tanzania wakiteseka.
Nape alisema Waziri Kawambwa naye anatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kuingia mkataba na kampuni ya ujenzi ya Progressive iliyopewa zabuni ya kutengeza barabara ya Natumbo hadi Tunduru wakati mkandarasi huyo hana uwezo wa kuijenga na matokeo yake amefukuzwa kazi.
Dk. Kawambwa ametupiwa lawama hizo kutokana na kuipa kazi kampuni hiyo wakati akiwa Waziri wa Miundombinu pamoja na kushindwa kusimamia elimu.
Akiwazungumzia Chiza na Malima, Nape alisema inasikitisha kuona wakulima wakiteseka, lakini waliopewa dhamana ya kuwasaidia wakishindwa kuwasikiliza na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao.
“Nitahakikisha mawaziri hao wanachukuliwa hatua ikiwa pamoja na kuwajibishwa na chama na ikishindikana tutatumia wabunge wetu kufanya kazi hiyo,” alisema Nape ambaye anaongozana na, Kinana, katika ziara ya kichama kwenye mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini.
Nape alisema akiwa katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kila eneo wananchi wanawalalamikia Chiza na Malima kwa mambo mbalimbali hivyo suala hilo linapaswa kufikia mwisho wake maana chama hakiwezi kuwavumilia.
“Katibu Mkuu (Kinana), nilimuuliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Chiza na Malima wamefika lini kusikiliza matatizo ya wakulima wa tumbaku, korosho na mahindi, alinijibu hakumbuki kama wamefika mkoani hapa. Nikafuatilia na kubaini si yeye tu hata Waziri aliyetangulia Profesa Jumanne Maghembe naye hakuwahi kufika. Najiuliza sababu nini, hakuna majibu,” alisema Nape.
Nape alisisitiza kuwa yuko tayari kupoteza nafasi aliyonayo kuliko kuacha Watanzania wakiendelea kuteseka kwa ajili ya mawaziri wachache waliopewa dhamana na Serikali ambayo ni ya CCM, lakini hawatimizi wajibu wao.
“Kwa hili hata chama changu na Katibu Mkuu mkiamua kunifukuza nipo tayari, ni bora nikawe mkulima, lakini kwa kuwa nafanya kazi ya kuwatetea wananchi watanilinda tu,” alisisitiza Nape.
Alitumia nafasi hiyo kumuomba Kinana apeleke ripoti ya mawaziri hao kwa CC wachukuliwe hatua na ikiwezekana waitwe wahojiwe.
Nape aliongeza: “Wananchi naomba mnilinde, lakini niseme ukweli. Mawaziri ambao tumewapeleka jikoni wameshindwa kupika chakula, tunasubiri sebuleni, lakini chakula hakiji. Wanatukwamisha, ni bora wakaondoka kama wameshindwa kazi.”
“Mimi ni kijana, sipo tayari kuona CCM inakuwa chama cha upinzani bungeni kwa sababu tu ya hawa wenzetu wachache ambao wanafanya makusudi na uzembe katika kutekeleza wajibu wao.
Kuhusu barabara ya kutoka Songea hadi Namtumbo, alisema anamshukuru Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa kumfukuza mkandarasi huyo, lakini
hiyo pekee haitoshi wale wote waliohusika kumpa mkataba wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa kuwa Serikali imepata hasara.
“Dk. Kawambwa amekuwa akitukwamisha CCM katika kutimiza wajibu wake. Hii barabara ya Namtumbo hadi Tunduru kushindwa kukamilika imeleta aibu kubwa na kututia fedheha. Hivyo lazima waliotoa mkataba wawajibishwe,” alisema Nape.
Kwa mujibu wa Nape, Dk. Kawambwa pia ameshindwa kushughulikia matatizo ya walimu nchini na kumkumbusha kuwa alipewa muda wa miezi sita na CCM na inakaribia kumalizika. Hata hivyo, hakufafanua miezi sita aliyopewa Waziri Kawambwa inahusu nini.
“Muda ukimalizika tutataka kufahamu yale ambayo tumeyaagiza kama yamefanikiwa na iwapo atakuwa ameshindwa ajue hatutakaa kimya,” alisema
Nape.
Alifafanua kuwa yeye (Nape) kama msemaji wa CCM kamwe hatakaa kimmya wakati chama kikipata aibu kwa kutotekelezwa miradi mbalimbali iliyoahidiwa katika Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.
Naye Katibu Mkuu Kinana alisema katika kikao cha CC kitakachofanyika mwezi ujao, kitamuandikia barua Rais Jakaya Kikwete ili mawaziri wake waende mbele ya kikao na kueleza kwa nini wasifukuzwe kwa kushindwa kazi.
Alisema kuwa haiwekani kuwa na Serikali ya walalamikaji kwa mfano mkuu wilaya analalamika, mbunge analalamika na kuweka wazi kuwa ni lazima yafanyika maamuzi magumu.
“Kama hali ndiyo iko hivi je, mwananchi wa kawaida atakwenda wapi. Hili sasa limefika mwisho, ni lazima wenzetu waliopewa dhamana wawajibike,” alisema Kinana.
Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa CCM kuwataja kwa majina mawaziri hadharani kueleza wazi kuwa wamshindwa kutimiza wajibu wao na kuwataka wang’oke madarakani.
Kadhalika, ni mara ya kwanza kwa Katibu Mkuu wa chama tawala kuinga mkono kutajwa kwa majina ya mawaziri hadharani na kueleza wazi kuwa watawashitaki kwenye chama na kuwataka wajieleze mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho.
Nape kushoto akiwa na Kinana |
Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete
............................................
Na Francis Godwin Blog
Na Francis Godwin Blog
MATEGEMEO yangu binafsi bila shaka ni mategemeo ya
watanzania wengi wapenda maende maendeleo wakiwemo hata wana chama
wa chama chao cha CCM na vyama vya upinzani kikiwemo Chadema ambao
nilipata kumsikia katibu mkuu wake Dr Slaa akiunga mkono kauli ya
katibu mkuu wa CCM Bw Kinana japo kwa mtazamo tofauti kwa kutaka
aliyewateuwa mawaziri mizigo pia ajiuzulu .
Yawezekana
kabisa wengi wetu tulitegemea ucheleweshaji wa uteuzi wa mawaziri
wanne waliotenguliwa nafasi zao na yule waziri wetu wa fedha Dr
Wiliam Mgimwa aliyefariki dunia ni kutokana na Rais wetu Jakaya
Kikwete kuangalia wabunge wenye sifa watakaoziba nafasi za hao
waliotenguliwa uteuzi wao na wale watakao shika nafasi za mawaziri
waliotajwa na chama kuwa ni mizigo .
Kwani
sikutegemea kuona mwenyekiti wa CCM Taifa Dr Kikwete akipuuza
kirahisi zaidi maoni ya katibu wake mkuu na katibu wake wa itikadi
na uenezi Bw Nape Nnauye ambao wamepata kuzunguka maeneo mbali mbali
ya Tanzania na kupokea maoni ya watanzania juu ya utendaji kazi wa
waziri mmoja baada ya mwingine na serikali kwa ujumla na hata kufikia
hatua ya kutumia majukwaa ya siasa ya CCM kuwataja kwa majina
waziri mmoja hadi mwingine jinsi gani walivyokuwa mzigo katika baraza
la mawaziri.
Wengi
wetu tulipokea kwa mikono miwili utendaji kazi wa katibu Kinana na
Nape na hata kupongezwa kwa kuliona hilo na huku tukisubiri nyufa
hiyo iliyojitokeza kuona inazibwa vema na mwenyekiti wa baraza la
mawaziri rais Kikwete ambae ndie aliwateua kumbe sio tulivyotegemea.
Ikumbukwe mawaziri waliotajwa kuwa ni mizigo ni pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza na Naibu wake, Adam Malima kuwa wameshindwa kazi na kupendekeza wang’olewe.
Kauli hiyo ambayo ilitolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, akisema kuwa mawaziri hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia Watanzania.
Alisema anasikitishwa na kitendo cha mawaziri hao waliopewa dhamana kushindwa kutambua wajibu wao na kwamba umefika wakati wa kuhojiwa na Kamati Kuu (CC) ya CCM ili wachukuliwe hatua kwani bila kufanya hivyo aibu itarudi kwa chama chake.
Nape alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wakati akielezea changamoto zinazowakabili wakulima ambao ni asilimia 80 ya Watanzania, huku mawaziri husika wakikaa kimya.
Alisema kuwa Waziri Chiza na Malima wamebaki wakifunga tai na kuvaa suti mjini wakati wakulima wa Ruvuma na mikoa mingine ya Tanzania wakiteseka.
Nape alisema Waziri Kawambwa naye anatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kuingia mkataba na kampuni ya ujenzi ya Progressive iliyopewa zabuni ya kutengeza barabara ya Natumbo hadi Tunduru wakati mkandarasi huyo hana uwezo wa kuijenga na matokeo yake amefukuzwa kazi.
Dk. Kawambwa ametupiwa lawama hizo kutokana na kuipa kazi kampuni hiyo wakati akiwa Waziri wa Miundombinu pamoja na kushindwa kusimamia elimu.
Akiwazungumzia Chiza na Malima, Nape alisema inasikitisha kuona wakulima wakiteseka, lakini waliopewa dhamana ya kuwasaidia wakishindwa kuwasikiliza na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao.
“Nitahakikisha mawaziri hao wanachukuliwa hatua ikiwa pamoja na kuwajibishwa na chama na ikishindikana tutatumia wabunge wetu kufanya kazi hiyo,” alisema Nape ambaye anaongozana na, Kinana, katika ziara ya kichama kwenye mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini.
Nape alisema akiwa katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kila eneo wananchi wanawalalamikia Chiza na Malima kwa mambo mbalimbali hivyo suala hilo linapaswa kufikia mwisho wake maana chama hakiwezi kuwavumilia.
“Katibu Mkuu (Kinana), nilimuuliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Chiza na Malima wamefika lini kusikiliza matatizo ya wakulima wa tumbaku, korosho na mahindi, alinijibu hakumbuki kama wamefika mkoani hapa. Nikafuatilia na kubaini si yeye tu hata Waziri aliyetangulia Profesa Jumanne Maghembe naye hakuwahi kufika. Najiuliza sababu nini, hakuna majibu,” alisema Nape.
Nape alisisitiza kuwa yuko tayari kupoteza nafasi aliyonayo kuliko kuacha Watanzania wakiendelea kuteseka kwa ajili ya mawaziri wachache waliopewa dhamana na Serikali ambayo ni ya CCM, lakini hawatimizi wajibu wao.
“Kwa hili hata chama changu na Katibu Mkuu mkiamua kunifukuza nipo tayari, ni bora nikawe mkulima, lakini kwa kuwa nafanya kazi ya kuwatetea wananchi watanilinda tu,” alisisitiza Nape.
Alitumia nafasi hiyo kumuomba Kinana apeleke ripoti ya mawaziri hao kwa CC wachukuliwe hatua na ikiwezekana waitwe wahojiwe.
Nape aliongeza: “Wananchi naomba mnilinde, lakini niseme ukweli. Mawaziri ambao tumewapeleka jikoni wameshindwa kupika chakula, tunasubiri sebuleni, lakini chakula hakiji. Wanatukwamisha, ni bora wakaondoka kama wameshindwa kazi.”
“Mimi ni kijana, sipo tayari kuona CCM inakuwa chama cha upinzani bungeni kwa sababu tu ya hawa wenzetu wachache ambao wanafanya makusudi na uzembe katika kutekeleza wajibu wao.
Kuhusu barabara ya kutoka Songea hadi Namtumbo, alisema anamshukuru Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa kumfukuza mkandarasi huyo, lakini
hiyo pekee haitoshi wale wote waliohusika kumpa mkataba wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa kuwa Serikali imepata hasara.
“Dk. Kawambwa amekuwa akitukwamisha CCM katika kutimiza wajibu wake. Hii barabara ya Namtumbo hadi Tunduru kushindwa kukamilika imeleta aibu kubwa na kututia fedheha. Hivyo lazima waliotoa mkataba wawajibishwe,” alisema Nape.
Kwa mujibu wa Nape, Dk. Kawambwa pia ameshindwa kushughulikia matatizo ya walimu nchini na kumkumbusha kuwa alipewa muda wa miezi sita na CCM na inakaribia kumalizika. Hata hivyo, hakufafanua miezi sita aliyopewa Waziri Kawambwa inahusu nini.
“Muda ukimalizika tutataka kufahamu yale ambayo tumeyaagiza kama yamefanikiwa na iwapo atakuwa ameshindwa ajue hatutakaa kimya,” alisema
Nape.
Alifafanua kuwa yeye (Nape) kama msemaji wa CCM kamwe hatakaa kimmya wakati chama kikipata aibu kwa kutotekelezwa miradi mbalimbali iliyoahidiwa katika Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.
Naye Katibu Mkuu Kinana alisema katika kikao cha CC kitakachofanyika mwezi ujao, kitamuandikia barua Rais Jakaya Kikwete ili mawaziri wake waende mbele ya kikao na kueleza kwa nini wasifukuzwe kwa kushindwa kazi.
Alisema kuwa haiwekani kuwa na Serikali ya walalamikaji kwa mfano mkuu wilaya analalamika, mbunge analalamika na kuweka wazi kuwa ni lazima yafanyika maamuzi magumu.
“Kama hali ndiyo iko hivi je, mwananchi wa kawaida atakwenda wapi. Hili sasa limefika mwisho, ni lazima wenzetu waliopewa dhamana wawajibike,” alisema Kinana.
Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa CCM kuwataja kwa majina mawaziri hadharani kueleza wazi kuwa wamshindwa kutimiza wajibu wao na kuwataka wang’oke madarakani.
Kadhalika, ni mara ya kwanza kwa Katibu Mkuu wa chama tawala kuinga mkono kutajwa kwa majina ya mawaziri hadharani na kueleza wazi kuwa watawashitaki kwenye chama na kuwataka wajieleze mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho.
Sasa
tujiulize kama Rais Kikwete katika uteuzi huu ameshindwa kuchukua
hatua na hata kuwapandisha vyeo mawaziri hao mizigo na kutoa kafara
kwa naibu wa elimu na mafunzo ya mafunzo Philip Mulugu na kumuacha
aliyetajwa boss wake Kawambwa ni kusema ushauri wa akina Kinana na
Nape umepuzwa ambao ni ushauri wa Chama cha CCM .
Ila
mbaya zaidi mbali ya kushindwa kuwawajibisha mawaziri hao mizigo
bado walioteuliwa ni heri hata ya waliokuwepo sasa katika uteuzi
huu kwa lugha nyepesi ni kusema tumeruka majivu na kukanyaga moto nini
hatima yake.
Pia
tujiulize hawa walkioteuliwa ni kwa ajili ya nani ni kwa faida ya
watanzania amao kuna jambo lipo nyuma ya pazia kweli kama mimi
ningetakiwa kutoa ushauri wa baraza basi lazima ningeanza na wale
waliotajwana chama kuwa ni mizigo kwa kuwaondoa kabla ya kuwaondoa
waliokwisha jiondoa akina Kagasheki na wenzake .
Ila
pia ushauri wangu kwa Kinana na Nape ni vema kabla ya kuanza
kukata tawi kuangalia wapi linaangukia na litachukuliwa baada ya
kuanguka ama litasimamishwa tena kwani ninachoona hata akina Kinana na
Nape wamepuuzwa na yawezekana wanaonekana kuwa na chuki binafsi na
waliowataja kuwa ni mizigo wakati yeye ameona si mizigo na kama Kinana
na Nape kweli wanaipenda kazi hiyo ni vema kwa heshima ya chama
kujiuzulu badala ya kuendelea kupokea fedheha na hata wakirudi
katika mikoa waliozunguka kutoka kauli ya kuwapinga mawaziri hao
yawezekana wakajishushia heshima yao .
Ushauri
wangu kwa Kinana na Nape kabla ya kutoa kauli nzito kama hizo kuuliza
misimamo ya viongozi wenu wa juu badala ya kugeuka kuwa ni
wavurugaji katika serikali na chama chenu na kama mnaona utafiti wenu
wa kuwa hao ni mawaziri mizigo ni wa
kweli basi chukueni hatua ya kujiuzulu
maana aliyewateua hajaona kuwa ni mizigo na hata kuwapuuza basi
mjue heshima yenu imeshuka maana mtaonekana ninyi ni watu wa majungu.
Post a Comment