Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATU 200 WAZAMA MTO NILE



Waliofariki walikuwa watu waliokuwa wanatoroka vita Sudan Kusini
Zaidi ya watu 200 raia wa Sudan Kusini wamezama katika ajali ya boti kwenye mto Nile wakikimbia vita vinavyoendelea katika mji wa Malakal.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Sudan Kusini.
Boti hiyo iliyozama, ilikuwa imewabeba watu wengi kupindukia. Watu hao walikuwa wanatoroka vita vinavyotokota katika mji wa Malakal.
Mapigano yalizuka Sudan Kusini mwezi Disemba mwaka jana baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake wa Rais Riek Machar, kwa kuwa na njama ya kumpindua.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa tangu ghasia kuanza nchini humo.Chanzo BBC Swahili
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top