Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ZIARA YA UJUMBE WA ALGERIA – MERERANI

 


4a
Meneja Mradi wa Kampuni ya TanzaniteOne Bw. Erenet Emmanuel Mtawali (mwenye kofia nyekundu) akiueleza ujumbe wa Algeria namna mitambo ya kusafisha na kuzalisha madini ya Tanzanite (haupo pichani) unavyofanya kazi.
………………………………………………………………………..
Ujumbe wa Algeria umepata nafasi ya kutembelea machimbo ya Tanzanite Mererani katika Kampuni ya TanzaniteOne ambapo walitembelea sehemu mbalimbali ikiwemo za uzalishaji, usafishaji, na uchongaji madini ya Tanzanite. Vilevile, wakiwa Mkoani Kilimanjaro walipata fursa ya kutembelea Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya kupandia cha Minjingu ambapo walijionea namna mbolea hiyo inavyozalishwa kwa kutumia masalia ya ndege aina ya Flamingo waliokuwepo eneo hilo miaka mingi iliyopita. Aidha, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea mbuga za wanyama katika bonde la ngorongoro ambapo wamehitimisha ziara yao nchini ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na nchi ya Tanzania katika sekta za gesi, mafuta,umeme na madini.

3
Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Sameja akiuongoza ujumbe wa Algeria kuondoka katika uwanja wa ndege wa Arusha , mara baada ya kumaliza ziara Mkoani humo. 2 (2)
Mtaalamu wa madini katika machimbo ya Kampuni ya TanzaniteOne Mererani Bw. Damian Mansala akiueleza ujumbe  wa Algeria namna mitambo ya kupeleka wachimbaji ardhini na namna mtambo huo unavyosafirisha mchanga wa madini uliochimbwa na kuusambaza katika hatua  mbalimbali za uzalishaji wa madini ya Tanzanite. 1Mkurugenzi Mkuu wa Migodi katika Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria Bw. Bourroudj Mohamed Tawar (aliyenyoosha mkono) akiangalia mwamba uliotokana na masalia ya ndege aina ya flamingo, yanayozalisha Mbolea ya kupanda ya Minjingu. Mwenye koti jeupe ni  Mkuu wa uzalishaji wa kiwanda cha Minjingu Bw. Inyana Mwambete, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho  Bw. Tosky Hans na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Samaje.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top