Na watenda kazi Francis Godwin Blog ,Njombe na Iringa
WAKATI wananchi wa kata ya Nduli jimbo la Iringa mjini na wale wa kata ya Njombe mjini jimbo la Njombe kusini kesho wanashiriki katika zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mdogo wa udiwani ,chama cha mapinduzi (CCM ) mkoa wa Iringa na Njombe kimelaani vurugu zinavyofanywa na viongozi na wafuasi wa Chadema katika chaguzi hizo na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo bila vitisho na kuchagua wagombea wa CCM.

Huku jeshi la polisi Imkoa wa
Njombe likidai limejipanga kwa ulinzi polisi mkoa wa Iringa limedai
kuwa kuna kikundi kinasakwa kwa kutaka kufanya vurugu katika
uchaguzi huo na kuwaondoa hofu wananchi kufika kupiga kura bila
kuogopa .
Kaimu katibu wa CCM mkoa wa
Iringa Hassan Mtenga alitoa kauli hiyo jana wakati wa ufungaji wa
kampeni za uchaguzi mdogo kata ya Nduli jimbo la Iringa mjini .
Alisema kuwa lengo la chama
chochote cha siasa ni kuona wananchi wake wanaendelea na shughuli
zao katika hali ya amani na utulivu na kuwa chama chochote cha
siasa kinachojihusisha na vitendo vya kinyama dhidi ya wananchi wake
ni wazi hakipo kwa ajili ya kulinda amani ya wananchi.
Hivyo alisema vurugu zilizofanywa
na wafuasi wa Chadema na mbunge wa jimbo hilo la Iringa mjini
mchungaji Peter Msigwa juzi ni wazi kuwa Chadema hakipendi kuna
wananchi wakifanya shughuli zao kwa amani na kutokana na unyama huo
unaofanywa na Chadema ni vema wana Nduli kuendelea kuchagua CCM ili
amani iliyopo izidi kulindwa .
Mtenga alisema mbali ya CCM kuruhusu vyama vingi vya siasa mwaka 1994 ila bado baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa ni mwanzo wa kuvuruga amani ya watanzania na kuwa ni vyama vya kusababisha vurugu hata mauwaji kwa watanzania .

Alisema kuwa haiwezekani kwa
chama makini chenye kupenda amani kuona kinashabikia vurugu na hata
wabunge wake na viongozi wake kila kukicha wakikamatwa kwa vurugu
katika mikutano.
Mtenga alisema jimbo la Iringa
mjini limeendelea kuzolota katika maendeleo kutokana na vurugu za
kisiasa za mara kwa mara zinazojitokeza na kuwa hata maendeleo
yanayoonekana kama huduma ya maji safi kwa wananchi wa Nduli ni
jitihada za mbunge wa wa CCM aliyekuwepo kabla ya Msigwa pamoja na
mbunge viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ambae kila wakati
bungeni amekuwa akipigania .
“Tunapenda kuwahakikishia wana Nduli kuwa iwapo mtatuwekea mrithi wa diwani marehemu Iddi Chonanga kutoka CCM pale alipoishia diwani wenu katika maendeleo pataendelezwa zaidi kwani mwenye kukabidhiwa mikoba ya diwani aliyekufa ni lazima awe kutoka CCM na si vinginevyo”

Kwa upande wake Chama cha
Mapinduzi mkoa wa Njombe kimeeleza kusikitishwa na vurugu mbali
mbali zinazojitokeza katika kampeni za udiwani kata ya Njombe mjini
baada ya wafuasi na viongozi wa Chadema kuwapiga wananchi .
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe
Deo Sanga ambae ni mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazin alisema kuwa
siasa inayofanywa na wana Chadema kwa Njombe mjini ni siasa ya kinyama
na kuwa ilipendeza kwa vyama vya siasa kushindana kwa sera na hoja
badala ya kushindana kwa vurugu .
HIvyo alisema kuwa ili CCM
kuendelea kutimiza ahadi zake na kuongoza kata hiyo ni wajibu wa
wananchi wa Njombe kuchagua mgombea wa CCM badala ya kuwasikiliza
wafuasi hao wa Chadema kutoka nje ya Njombe ambao wapo kwa ajili ya
kutaka kuvuruga uchaguzi huo.
Huku mbunge wa jimbo la Ludewa
Deo Filikunjombe akiwataka wana Njombe mjini kutokubali kata hiyo
ya Njombe mjini kuchukuliwa na vyama vya upinzani na kuwataka
kuchagua chama cha mapinduzi.
Filikunjombe alitoa kauli hiyo
wakati wa kumnadi mgombea udiwani wa CCM katika kata hiyo ya Njombe
mjini na kuwa Wilaya ya Ludewa na Njombe ni wilaya majirani na kuwa
masilimali za Ludewa ambazo ni makaa ya mawe na Liganga si tu ukombozi
kwa wana Ludewa ni ukombozi wa mkoa wa Njombe na Taifa hivyo
kuwataka vijana kuendelea kuwa na imani na serikali ya chama cha
mapinduzi chini ya Rais Dr Jakaya Kikwete ambae katika utawala wake
watanzania wanashuhudia miradi hiyo mkikubwa inaanza.
Alisema kuwa uchumi wa Njombe na
Ludewa baada ya kuanza kwa miradi hiyo utakuwa zaidi kutokana na
vijana wengi kupata ajira katika miradi hiyo.
Wakati huo huo Jeshi la polisi mkoa wa Njombe na Iringa limesema limejipanga vyema kwa ulinzi wakati wa zoezi nzima la upigaji kura hadi kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi na kuwa atakayejaribu kumtisha mpiga kura asifike kupiga kura atakiona cha moto kutoka kwa jeshi hilo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa
Njombe Fulgence Ngonyani akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa
njia ya simu jana alisema kuwa jeshi lake limefanikiwa kuwapa
mafunzo maalum askari wake kwa ajili ya kulinda amani wakati wa zoezi
la uchaguzi huo na kuwataka wananchi wa Njombe mjini wenye sifa ya
kupiga kura kufika kupiga kura bila kitisho kutoka kwa mtu yeyote na
kuwa yule atakayetishwa asisite kutoa taarifa kwa askari
watakaokuwepo maeneo yanayozunguka vituo vya kupigia kura.
Huku kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akisema kuwa jeshi lake limejipanga toka mwanzo katika kampeni hizo.
Kamanda Mungi alisema kuwa
kumekuwepo na vurugu za hapa na pale ambazo zinatokana na pambe moja
kati ya zinazovutana kukata tamaa katika uchaguzi huo kutokana na
kujijipanga vema japo wao kama polisi wamejipanga kuona amani na
utulivu unakuwepo wakati wote wa upigaji kura na utangazaji wa matokeo
japo alisema zipo taarifa za baadhi ya wafuasi wa moja kati ya
vyama vya siasa kupanga kufanya vurugu na kuwa tayari kikundi
hicho kinajulikana na wameanza msako wa kukisaka ili kufikishwa
katika vyombo vya sheria.
Joto hilo la uchaguzi mdogo
katika kata ya Nduli linaonyesha kwenda vibaya zaidi kwa Chadema
kutokana na mgombea aliyesimamishwa Ayub Mwenda awali alipata kuwa
mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nduli na kutolewa na wananchi
kwa kura za maoni za kutokuwa na imani nae kutokana na madai ya kula
fedha za kijiji na baada ya hapo kuamua kuhamia Chadema na kuchukua
fomu ya kuwania nafasi hiyo ya udiwani jambo ambalo wanadai kuwa
kupata udiwani katika kata hiyo ni vingumu zaidi .
Pia uchaguzi huo ni kipimo moja
wapo kwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kama
bado anakubalika ama lah ila pia ni kipimo kwa CCM kuendelea
kushinda chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015 .
Hali katika kata ya Njombe mjini
upepo wa kisiasa hadi sasa ni 50 kwa 50 kwa vyama viwili
vilivyojitokeza CCM na Chadema ambapo kuna uwezekano wa CCM kushinda
tena kwa kumrudisha diwani wa CCM ama kushindwa kutokana na vyama
hivyo viwili kuonyesha kukamiana kupita kiasi.
Post a Comment