Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero Mh Anthony Mtaka Akijaribu Kuwatuliza wakulima hao
bila Mafaniko na Ndipo Ilipotolewa Amri ya Kuwatawanya Kwa kutumia
Mabomu Ya Mabomu.
Baadhi
ya wananachi wa kijiji hicho wakimzonga mkuu wa Wilya ya Mvomero
Anthony Mtaka [mwenye shat la damu ya mzee] huku mkuu wa polisi Wilaya
ya Mvomero OCD ldd Abdallah lbrahim akimlinda
Wananchi hao walikamatwa wakidaiwa kuwapiga mawe polisi wakati walipofyatua magomu ya machozi
NA DUSTAN
KWA
mara nyingine tena leo mamia ya wakulima wamefunga barabara kuu ya
Morogoro-Iringa Kijiji cha Mangae wilayani Mvomero Mkoani hapa,baada ya
kundi la wafugaji jamii ya Wamasai kuwavamia mashambani na kuwapiga
wakulima kilichosababisha kujeruhiwa vibaya wakulima watano.
Kwamijibu
wa mashuhuda Amina Kitengule dada wa majeruhi Rashi Abdalah mwenye hali
mbaya ambaye ni miongoni mwa majeruhi watano waliolazwa hospitali ya
rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambaye anadaiwa kuharisha na kutapika Damu
kutokana na kipigo hicho,alisema kaka yake huyo alikumbwa na mkasa huo
jana jioni wakati akianda shmba lake msimu huu wa kilimo.
Amina
alisema siku ya tukio wakulima wakiwa shamba lilitokea kundi la
wafugaji jamii ya Wamasai wakiwa na aina mbalimbali za sialaha za jadi
na kuanza kuwachapa wakulima hao waliokuwa mashmbani.
“sisi
hapa tunalima katika kitongoji cha Mkangazi,kwa muda mrefu tumekuwa na
tatizo hili la kuvamiwa na wafugaji na kupigwa kisha kujeruhiwa nakila
tukitoa taarifa serikalini hazifanyiwi kazi”alisema Amina na kuongeza
“mfano
jana jioni walitokea tena hao Masai na kumvamia kaka yangu akiwa
analima,wakamny’ang’anya jembe na na kuanza kumpiga nalo kwenye makalio
walipoona hawaridhiki na kipigo hicho wakaanza kumchoma na mkuki…sasa
hivi anaharisha na kutapika damu hospitali ya mkoa”
Mbali
na kupigwa Rashid Abdalah,inasadikiwa zaidi ya watu watano walipigwa
katika maeneo tofauti na kujeruhiwa vibaya kwenye miili yao kabla
hawajakimbizwa hospitali ya rufaa kwa matibabu.
Kufuatia
kuenea kwa taarifa za wakulima hao kupigwa na wafugaji, kuanzia saa 2
asubuhi wakulima walijikusanya na kuamua kuziba barabara hiyo kwa lengo
la kushinikiza mkuu wa mkoa Dk Joel Bendera kufika hapo kutatua mgogoro
huo.
Kwa
mujibu wa wakulima hao uamuzi wa kumwita mkuu huyo ni kutokana shutuma
za kukithiri kwa rushwa kwa viongoizi wa wilaya hiyo jambo ambalo
limekuwa linalea na kuukuza mgogoro huo sambamba na kuwatia hasara na
vilema visivyo tarajiwa.
“hatufungui
barabara mpaka mkuu wa mkoa aje maana hatuana imani tena na uongozi
wote wa wilaya”walisikika wakisema baadhi ya wananchi hao muda mfupi
baada ya mkuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama kufika eneo hilo.
Akiwasihi
kufungua barabara hiyo kwa madai kuwa atalishugulikia suala hilo kwa
kuwakutanisha wakulima na wafugaji,Mkuu wa wilaya hiyo akiwa juu ya gari
la polisi alisema kiliochao kimesikika na anaahidi kutafuta ufumbuzi
mapema iwezekanavyo.
Hata
hivyo wakulima hao walikataa kufungua barabara hiyo na kuendelea
kuchochea moto kwa kumwagia mafuta ya petrol kwenye mataili ya magari
yaliyokuwa yamepangwa barabarani.
Kufuatia
kukaidi kwa agizo hilo na kuendelea kuchomwa moto mataili hayo,Kamanda
wa polisi mkoa wa Morogoro,Faustine Shilogile alilazimika kufika eneo
hilo na kuagiza polisi waliokuwa eneo hilo kuwatawanya kwa kupiga risasi
za moto hewani.
Hata
hivyo kama sia jajizi wakulima hao walikaidia na kuanza kuwapopoa kwa
mawe polisi na viongozi waliokuwa eneo hilo jambo lililomlazimu Kamanda
Shilogile kuagiza kupiga mabomu ya machozi yaliyosaidia kuwatawanya na
kufunguliwa kwa barabara hiyo.
Juhudi
za kuupata uongozi wa hospitali ya rufaa Morogoro juu ya majeruhi wa
mapigano hayo hazikuweza kufanikiwa kutokana na uongozi huo kudaiwa kuwa
nje kwa kazi za kiofisi.


Post a Comment