Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAGEREZA MKOA WA TANGA YAANZA MAANDALIZI YA UKARABATI WA OFISI MPYA ZA UTAWALA, JIJINI TANGA

 
image
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya(wa pili kulia) akielezea hatua mbalimbali za Maandalizi ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga(wa kwanza kulia) ni Afisa Habari wa Jeshi la Magereza, Mkaguzi wa Magereza Deodatus Kazinja alipotembelea kujionea hatua mbalimbali za ukarabati unaoendelea leo Februari 7, 2014 Jijini Tanga.
image_1Muonekano wa mbele wa Jengo la Kikoloni ambalo linalotarajiwa kukarabatiwa kwa ajili ya Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga. Jengo hilo hapo awali lilitumika kama Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Tanga ambapo hivi sasa Jeshi la Magereza tayari limeanza ukarabati wa jengo hilo. Wa kwanza katika picha ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya akiwa ameongozana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza leo Februari 07, 2014 Jijini Tanga.
image_2
Tofali ambazo zimefyatuliwa kwa ajili ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga. Ukarabati huo wa Ofisi mpya za Utawala unaanza hivi karibuni Jijini Tanga na utasimamia kwa karibu na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga.
image_3
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya akiongoza Kikao kazi Ofsini kwake pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wanaofanya kazi Ofisi ya Magereza Mkoa wa Tanga leo Februari 07, 2014 alipotembelewa Ofsini kwake na timu ya Maafisa Habari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaaam(hawapo pichani) photo
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wanaofanya kazi Magereza Mkoa wa Tanga baada ya kutembelea sehemu mbalimbali ya maandalizi ya ukarabati wa Ofisi  Mpya za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga leo Februari 07, 2014(wa Nne kulia) ni Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Augustino Mboje(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top