Makamo
mwenyekiti wa CCm Taifa Philipo Mangula akivishwa skafu na chipukizi
baada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Morogoro.
Makamo mwenyekiti huyo akisalimiana na mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Morogoro Juliana Mwenda.
makamo huyo akisalimiana na katibu wa UVCCM mkoa wa Morogoro Nicodemas.
Makamo huyo akiongea na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Morogoro pamoja na wa wilaya ya Morogoro mjini.
Hayo ni mapokezi aliopata alipoingia katika kata ya Rudewa wilaya ya Kilosa
Mangula akifungua shina la wakereketwa la Njia panda katika kata hiyo ya Rudewa
Maelfu waliofurika katika kata hiyo wakati wa kampeni ya udiwani ya Rudewa.
Mangula akiwa na mgombea wa udiwani kata ya Rudewa Subiri Joseph.
Habari zaidi soma hapa chini.
MAKAMO
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Taifa Philipo Mangula amesema kuwa
muda wa kampeni za Urais,udiwani, ubunge na hata nafasi za serikali za
mitaa bado na kwamba wanaofanya kampeni wanakiuka katiba na kanuni na
hivyo CCM inatambua mitandao yote na itawashughulikia.
Alisema
hayo Februari 8 mwaka huu wakati akiongea na viongozi wa wilaya na mkoa
wa Morogoro alipofika kwajili ya kampeni za Uchaguzi mdogo wa udiwani
katika kata za Ludewa wilayani Kilosa na Tungi Manispaa ya Morogoro.
Alisema
kuwa tayari walishafungua mafaili ya watu hao wenye mitandao ya kampeni
na kwamba wanatambua mitandao yote hata katika ngazi za mikoa na
watawashughulikia.
Alisema
kuwa Rais, wabunge na madiwani waliopo madarakani bajeti yao ya
mwisho inashia mwezi Juni 2015 na kwamba wanaojitokeza sasa ni
waharifu na lazima wachukuliwe hatua.
Aidha
alisema kuwa Viongozi waliopo madarakani wanahaki zote na kwamba ni
lazima walindwe ili waweze kufanya kazi zao vizuri bila kunyanyasika na
kwamba kuanza kampeni hizo kunafanya kuwavunja nguvu viongozi hao.
‘’Mara
zote tatizo la kuanzisha makundi kabla ya kampeni ni kusababisha chuki
na uhasama na kupelekea makundi hayo kurushiana maneno, na hiyo
inasababisha hata nchi kushindwa kutaalika’’ Alisema
Aliwataka
viongozi kutengeneza mitandao ya kuwafutilia watu hao wenyekufanya
kampeni za chini kwa chini kinyume na taratibu na kukabiliana nazo .
‘’ Ni mwiko kwa mtu kuunda vikundi na kufanya kampeni za chini kwa chini , tutakabiliana nazo’’ alisema.
Alisema
kuwa suala la kutangaza nia ya kutaka kugombea nafasi yeyote sio kosa
bali kuanza kampeni ndio kosa kubwa kimaadili ya chama.
Kwa
upande mwingine Mangula alisema kuwa wabunge na madiwani kufanya zaira
za mara kwa mara ni sawa na mkulima kupalilia shamba lake hivyo
wanaodharau kufanya hivyo wasije kulaumu na kwamba watavuna
walichopanda.
‘’ Ni
dhambi kubwa kwa mbunge kutotekeleza ahadi zake, ni sawa na mkulima
kupanda mbegu pasipo kufanya palizi, akikuta mazao yake yameliwa na
magugu atamlaumu nani’’ Alisema.
Kwa
upande mwingne Mangula alisema kuwa nia ya mwenyekiti wa CCm taifa Rais
jakaya Kikwete ni kuhakikisha katiba inakamilika haraka ili itumike
katika uchaguzi ujao.
Alisema
kuwa itakuwa vema ndani ya siku 70 zilizopangwa kwaajili ya bunge la
katiba ikakamilika na kurejeshwa kwa wananchi ili kutimiza malengo
yaliokusudiwa.
Awali
katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli alisema kuwa wapo baadhi ya
viongozi walionuna baada ya majina walioyataka kurejeshwa katika
uchaguzi huo kutorudi na hivyo kususia kampeni jambo ambalo Mangula
alisema kuwa si dhambi kurejeshwa kwa mgombe wa nafasi ya 3
kinachozingatiwa ni vigezo.
Pia alisema kuwa katika kata ya Ludewa wananchi wake wanalalamikia mbunge wao Mustapha Mkulo kutotimiza ahadi alizoahidi.










Post a Comment