Mwanariadha
wa Marekani Sage Kotsenburg amekuwa mwanariadha wa kwanza kunyakua
medali ya kwanza ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya Majira ya
Baridi inayofanyika katika mji wa Sochi nchini Urusi.
Sage
Kotsenburg, amenyakua medali hiyo katika mchezo wa kuteteleza katika
barafu kwa kwa kutumia ubao kwa upande wa wanaume, ukiwa ni mmoja katika
michezo 12 mipya iliyoingizwa katika michuano hiyo, ili kuwavutia
vijana.
Mwanamke
wa kwanza kushinda medali ya dhahabu ni Marit Bjoergen wa Norway,katika
mbio za marathon za kilomita 15. Umati mkubwa wa mashabiki wa Uholanzi
wanatarajiwa kumshangilia bingwa mtetezi wa mchezo wa kuteleza katika
barafu, Sven Kramer, akijaribu kutetea taji lake kwa upande wa wanaume
mita elfu tano.
Rais
Vladmir Putin wa Urusi alifungua rasmi jana(Ijumaa), mashindano ya
Olimpiki ya majira ya baridi katika mji wa utalii wa Sochi katika
sherehe zilizofana.
Waliokuwa
wanariadha mashuhuri nchini Urusi waliubeba mwenge wa Olimpiki kabla ya
kuwashwa na aliyekuwa mlinda lango wa mchezo wa magongo Vladislav
Tretiak pamoja na mchoraji wa barafu Irina Rodnina.
Katika
siku 16 zijazo,karibia wanariadha 3000 watashiriki katika michezo
mbalimbali 98 katika mashindano hayo yaliodaiwa kugharimu takriban dola
billioni 50.Chanzo BBC Swahili
Post a Comment