INAWEZA
kukushtua lakini ndivyo ilivyotokea. Kichanga cha siku thelathini, Veis
Venus kiliibwa hivi karibuni, mtuhumiwa akiwa ni mwanamke aliyetajwa
kwa jina moja la Grace wa ni mjamzito feki.Mtoto Veis Venus aliyekuwa ameibiwa
Tukio
hilo la kushangaza lilijiri Januari 27, 2013 maeneo ya Posta jijini Dar
na mtoto huyo kupatikana Januari mwaka huu, mkoani Mbeya.
Akizungumza
na waandishi wetu juzi nyumbani kwake, Kawe ya Tanganyika Parkers, Dar,
mama mzazi wa mtoto huyo, Salma alisimulia kisa kizima:
“Ilikuwa Januari 24, mwaka jana, marafiki zangu watatu walikutana na mwanamke aliyesema ana taasisi inayotoa misaada kwa watoto.
“Kwa
sababu nilihitaji, nikambeba mwanangu na kwenda Mwenge ambako nilionana
na mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Grace.

Mama akiwa na mwanaye Veis Venus.
“Aliniambia asingetoa msaada mpaka Sikukuu ya Krismasi na Boxing Day zipite. Januari 27 nikakutane naye.
”Cha kushangaza siku hiyo sikumkuta Grace bali mwingine aitwaye Suzana. Alisema ni mfanyakazi wa Grace.
“Siku
hiyo nilikuwa na mwanamke mwingine naye ana mtoto. Suzana akatuambia
wana ofisi Mlimani City na Posta, hivyo tulitakiwa kwenda Posta kupokea
misaada hiyo.
“Kufika kituoni, Suzana akashauri mimi na mwenzangu tupande daladala, yeye na watoto wetu wapande Bajaj tukakutane Posta.
“Dakika chache mbele akabadili kauli, akasema yeye aondoke na mtoto mmoja tu na alimchagua mwanangu.

Mama mtoto.
“Tulipanda
daladala mpaka Posta ambapo tuliwasiliana na Suzana akasema yupo kwenye
foleni. Tulimsubiri kwa muda, tulipompigia tena simu yake ikawa
haipatikani.
“Ilibidi
tumpigie simu Grace, akasema Suzana alipitia Kigamboni kuchukua misaada
hivyo tumsubiri. Tuliendelea kusubiri hadi saa kumi na mbili jioni,
hakuna aliyekuwa akipatikana kwenye simu,” alisema Salma.
Salma:
Nililia sana jamani! Nilisema moyoni sitaki tena msaada namtaka mtoto
wangu lakini hakuwepo. Niliwapa habari ndugu kisha tukaenda kutoa
taarifa Kituo cha Polisi cha Kawe na Kituo cha Polisi Sitakishari jijini
Dar kwa vile mtu wa kwanza kuniambia habari za msaada anaishi huko.
Naye shangazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Selina alikuwa na haya ya kusema:
“Baada ya kupokea habari kutoka kwa Salma tulichukua namba za wale wezi na kwenda nazo kampuni moja ya simu kuziangalia.
“Desemba
30, mtu wa kampuni hiyo aliwaambia polisi, Suzana yupo Mbeya. Januari
18, bila kutarajia, Grace na Suzana wakatiwa mbaroni huko Mbeya. Grace
alidai eti mtoto ni wake.
“Januari 19, polisi waliwachukua wote na kurudi nao Dar kwa ajili ya vipimo vya DNA vya Grace, Salma na mtoto Veis.
“Baada
ya vipimo, majibu yalionesha mtoto ni wa Salma huku Grace na Suzana
wakiwekwa chini ya ulinzi wa polisi na kufanya taratibu za kuwafikisha
mahakamani kujibu tuhuma hizo,” alisema Selina


Post a Comment