
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala akimtwisha maji mama mara baada ya kufungua mradi wa maji Kagugu.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla akizungumza na katika Ofisi za Mkuu wa
Mkoa Morogoro mara baada ya kuanza ziara yake Mkoani Morogoro, na kulia
ni Mkuu wa Morogoro, Joel Bendera.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akiwa na mkandarasi katika kituo cha kusafishia maji cha Mifiga.
Kituo cha kusafishia maji cha Mmbogo kikiwa katika muendelezo wa ujenzi.
********
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla ameanza ziara yake mkoani Morogoro Jumatano kwa kutembelea Mamlaka ya Mazingira na Majisafi Morogoro (MORUWASA). Mhe. Makalla alifika MORUWASA na kujionea utendaji na kupata taarifa ya mamlaka hiyo ambayo inatoa huduma ya maji mjini Morogoro na kukagua miradi inayotekelezwa mkoa huo.
“Ninawaagiza wakandarasi wahakikishe wanarudi kwenye maeneo yao ya kazi mara moja, kama Waziri Maghembe alivyoagiza. La sivyo Serikali itaangalia taratibu na kuchukua hatua kali. Na mkandarasi atayekaidi hatapata kazi sio tu Wizara ya Maji, bali Tanzania nzima”, alionya Naibu Waziri.
“Muwe karibu na kuwahudumia vizuri wateja na kuwe na ratiba nzuri ya mgao na ya kueleweka na kwenye dharura mfike mara moja bila kuchelewa. Muondoe urasimu usio wa lazima katika kutoa huduma kwa wananchi wote”, alisema Makalla.
Pia, alisema wananchi waiunge mkono Serikali katika kutunza mazingira na vyanzo vya maji na amekuja Wizara ya Maji kutimiza sera za maji na mipango ya Serikali katika sekta hiyo na si vinginevyo. Na kuahidi kuwasilisha maombi yote aliyoyapokea Wizarani na kuyapapa msukumo yafanyiwe kazi, isipokuwa yale yaliyo ndani ya uwezo wao wafanye bidii kuyatatua.
Naibu Waziri Alhamisi aliendelea na ziara hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na kukagua baadhi ya miradi ikiwemo Kibati, Kwadoli na Kagugu. Vilevile, ametembelea bwawa la Mindu na kijijiji cha Lusungu.




Post a Comment