Ubalozi
wa Jamhuri ya Indonesia kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, unapenda kuvijulisha vyombo vyote vya habari
nchini kuwa kutakuwa na Mkutano wa pili wa ushirikiano baina ya nchi za
Mashariki mwa Asia kuhusu Maendeleo ya Palestina (2nd
Conference of Cooperation among East Asian Countries for Palestinian
Development – CEAPAD II) ambao utafanyika Jakarta, nchini Indonesia
kuanzia tarehe 28 Februari hadi tarehe 2 Machi 2014.
Vyombo vya Habari vitakavyopenda kushiriki mkutano huo viwasiliane na Ubalozi wa Jamhuri ya Indonesia nchini.
Imetolewa na:
Idara ya Habari – MAELEZO
Post a Comment