Na Mwandishi Wetu
TAASISI inayoshughulika na kilimo cha maua na mboga
mboga nchini (TAHA) imemteua Bw. Eric Ng'imaryo kama Mwenyekiti wake mpya
kuchukua nafasi iliyoaachwa wazi na Bw. Colman Ngalo, ambaye
ameiendesha taasisi hiyo kwa mafanikio kwa takribani miaka kumi ya utawala
wake.
Sambamba na uteuzi huo pia Bw. Ng'imaryo, pia taasisi hiyo
ilimpata Makamu Mwenyekiti mpya pamoja na wajumbe nane wa Bodi ya TAHA
pia walichaguliwa katika Mkutano Mkuu wa TAHA (AGM) uliofanyika
hivi
karibuni jijini Arusha.
Miongoni mwa wanaounda Bodi mpya ya
taasisi ya TAHA ni pamoja na: Bi.
Fatma Riyami , Bw. Ravi Bhalerao, Bw.
Herald Peeters , Bw. Juma
Lossini , Bw. Robert Daniel, Bw. Tjerk Scheltema na
Bw. Adrian Moss.
Bw. Juma Ally Juma amechaguliwa kama mwakilishi kwenye
taasisi ya Bodi
ya TAHA kutoka jimbo la uchaguzi Zanzibar.
Taasisi hiyo ya
TAHA kwa sasa imekuwa ikikuza msendeleo ya wakulima
nchini ambayo hatua
inayoonesha kujitolea katika kukuza maendeleo ya
sekta ya maua na mboga mboga
nchini.
Kablya ya uteuzi huo, Bw. Ng'imaryo alikuwa Mwenyekiti wa
Arusha
Blooms Company Limited, kampuni ambayo ni mwanachama wa TAHA na
moja
ya wazalishaji wakubwa wa mboga mboga nje ya nchi na nchini.
Bw.
Ng'maryo kitaalamu ni mwanasheria ambaye amekuwa akifanya kazi zake
za
kisheria katika Tanzania tangu mwaka 1987. Hata hivyo, Mwnyekiti
huyo
mpya ni mfanyabiashara, mkulima na mwandishi mahiri.
"Nimepata
heshima kubwa na ya kipekee kabisa kuweza kuchaguliwa kuwa
Mwenyekiti mpya wa
TAHA na niuangalia uteuzi huu kutekeleza wajibu na
majukumu kwa kufanya kazi
na Bodi na Sekretarieti ili kuhakikisha
kwamba dira yetu inatekelezwa. Nami
nitakuwa sehemu ya kuifanya
taasisi yetu ya TAHA kuwa na mafanikio zaidi
katika siku zijazo.
Ninapenda pia kuwashukuru Bw. Colman Ngalo, Mwenyekiti
anayemaliza
muda wake, kwa uongozi wake mzuri.
Bw. Ngalo amekuwa
nguzo ya TAHA kwa miaka kumi iliyopita. "Bw.
Ng'imaryo pia alitoa shukrani
zaidi kwa Bi. Jacqueline Mkindi ,
Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA, samabmba na
Sekretarieti nzima ya TAHA
kwa mchango wao mkubwa kwa taasisi na sekta nzima
ya maua na mboga
mboga. "Jacqueline amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa mfano.
Utendaji wake
wa kazi umeijenga taasisi yetu uaminifu na heshima kutoka kwa
Serikali
na Washirika wa Maendeleo."
Katika hotuba yake, Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake, Bw. Ngalo
ameusifu uamuzi wa TAHA wa kuweza kumchagua
Bw. Ng'imaryo ambapo
ameleelezea kuwa na imani na uongozi wake ambao utaleta
mageuzi ya
kweli kwenye sekta ya maua na mboga mboga. "Kwa niaba ya Bodi ya
TAHA
inayomaliza muda wake, napenda kumpongeza Bw.Eric kwa
kuchaguliwa
kwake kuwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TAHA na ni mategemeo yangu
kuwa
tutaendelea kufanya kazi pamoja naye katika miaka
ijayo.
Mchanganyiko wa ujuzi wake katika sekta ya maua na mboga mboga
na
uzoefu mkubwa sambamba na utaalamu unafanya kuwa mtu bora
kuchukua
nafasi ya Uenyekiti wa TAHA na sekta yenye maendeleo endelevu.
Napenda
pia kuishukuru Sekretarieti ya TAHA na wanachama wake kwa
ushirikiano
wao bora katika muongo uliopita. Kwa ushirikiano tumepata
mafanikio
mkubwa. Mimi ninajisikia fahari kubwa kukabidhi taasisi hii
yenye
mafanikio ambayo bado ina fursa kubwa kwa ukuaji zaidi katika TAHA
na
sekta nzima kwa ujumla."
TAHA ni taasisi ambayo ni mwanachama wa
sekta binafsi ambapo imekuwa
ikishiriki kwa ufanisi katika kubadilisha kilimo
cha sekta ya maua na
mboga mboga toka kuanzishwa kwake mwaka
2004.
Kutokana wa hatua za uwepo wa TAHA , sekta ya maua na mboga
mboga
nchini na kufanikiwa kuvutia washirika mbali mbali kutoa
misaada
mikubwa ikiwa ni pamoja na serikali ya Tanzania na Washirika kama
vile
USAID, BEST- AC, Ubalozi wa Uholanzi , ITC, na Serikali
Finland.
TAHA inatoa sapoti mbali mbali kwa wadau wa sekta ya maua na
mboga
mboga ikiwemo kuwajengea uwezo kwenye majukwaa, kulinda na
kukuza
maslahi ya watendaji katika sekta hiyo ya maua yaani wazalishaji
,
wauzaji, wasindikaji, na watoa huduma ya maua, matunda , mboga, viungo
,
mimea na mbegu za maua.
MWISHO
on Sunday, February 9, 2014
Post a Comment