Baadhi
ya wanafunzi w shule ya awali ya Kilimani wakiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya wageni waliowatembelea kuwafundisha swala zima la usafi
shuleni hapo kupitia miradi ya Mikono Ming’avu (MiMi) na Kinywa Kisafi
(KiKi) chini ya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Aspiration
Initiatives – TAI.
Wanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Kilimani wakijifunza kwa vitendo jinsi ya kusafishwa kinywa na kuepukana na magonjwa yanayotokana na kutosafisha kinywa.
Katibu
Mkuu wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Aspiration Initiatives -
TAI Bw. Gwamaka Mwabuka akitoa maelekezo kwa mwanafunzi wa darasa la
pili shule ya Msingi Kilimani Juma Abdul jinsi ya kunawa mikono kwa
usahihi ili kuipeka magonjwa. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wanafunzi toka
Denmark waliopata mualiko na TAI kupitia taasisi ya Global Platform.
Taasisi
isiyo ya kiserikali ya TAI - Tanzania Aspiration Initiatives imefanya
mafunzo ya kulinda afya kwa vitendo kwa wanafunzi Zaidi ya 200 wa Darasa
la Kwanza, la pili na darasa la awali katika shule ya msingi Kilimani
iliyopa Sinza Uzuri wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni
muendelezo wa miradi miwili inayojulikana kama Mikono Ming’avu (MiMi) na
Kinywa Kisafi (KiKi).
Miradi
yote ina lengo kuu la kupambana na magonjwa yanayoweza kuzuilika kama
Magonjwa ya tumbo na yale ya meno na kinywa yanayoathiri zaidi watoto.
Mafunzo hayo pia yalishirikisha Vijana wengine kutoka nchini Denmark
walio nchini katika ziara ya kimasomo chini ya Jukwaa la kimataifa la
Global Platform.
Mikono
Ming’avu (MiMi) ni mradi uliyojikita katika kutoa mafunzo kwa vitendo
kwa watoto wa shule za msingi kutatua tatizo la magonjwa
yanayosababishwa na mikono michafu kama vile Pneumonia na homa ya
Matumbo (Diarrhea). Mradi huu tayari umeshawafikia Zaidi ya watoto 1000
katika baadhi za shule za msingi jijini Dar es salaam huku malengo ni
kufikia shule zote za msingi Tanzania nzima.
"Hatua
hizi za TAI ni baada ya kuona Watanzaia wengi hawana tabia ya kunawa
mikono na sabuni kwa ufasaha ambapo ni moja ya sababu inayochangia
magonjwa yanayoweza kuzuilika, lakini pia yanaathiri ukuaji wa mtoto.
Kila mwaka watoto Zaidi ya milioni 3.2 duniani walio chini ya miaka 5
wanakufa kwa sababu ya homa ya matumbo na pneumonia yakiwa ni magonjwa
yanayoongoza kusababisha vifo kwa watoto baada ya malaria hasa katika
nchi za kusini mwa jangwa la sahara, Tanzania ikiwepo" alisema Bw.
Gwamaka Mwaibuka, Katibu Mkuu wa TAI.
Kinywa
Kisafi (KiKi) ni ni moja kati ya mradi ya TAI ukiwa na lengo la
kupunguza tatizo la magonjwa ya Kinywa na meno kwa watoto ambapo taasisi
hiyo hufanya mafunzo kwa vitendo kwa kushirikiana na wataalam
kuwafundisha watoto njia sahihi za kufanya usafi wa meno na kinywa na
kuhimiza tabia ya kusafisha kinywa kuanza tangu utotoni.
TAI
ni taasisi iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha maisha ya kila mmoja
katika jamii hasa watu wanaoushi katika mazingira magumu na umasikini
kupitia sekta tano za Elimu, Afya, Ujasiriamali, Teknolojia ya Habari na
Mazingira. Kwa taarifa Zaidi ingia www.tai.or.tz au Tufuate katika ukurasa wetu wa Facebook www.facebook.com/tai2012.
Post a Comment