Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TFF YAZITILIA UBANI YANGA NA AZAM MICHUANO YA AFRIKA


Na Boniphace Wambura, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri klabu za Yanga na Azam ambazo timu zake zinatuwakilisha kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Kombe la Shirikisho (CC).
Yanga inacheza na Komorozine ya Comoro katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya CL itakayochezwa kesho (Februari 8 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nayo Azam inaikaribisha Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya CC utakaochezwa Jumapili (Februari 9 mwaka huu) saa 10 kamili kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Kila la heri; Kikosi cha Yanga SC ambacho kesho kitamenyana na Komorozine 

Ni matumaini yetu kuwa timu hizo mbili zitatuwakilisha vizuri kwenye michuano hiyo, na kuwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi viwanjani kuziunga mkono hasa kwa vile zinacheza nyumbani.
Wakati huo huo: Timu ya taifa ya soka ya wanawake ‘Twiga Stars’, imehamishia kambi yake jijini Dar es Salaam kutoka Mlandizi mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya michuano ya Afrika (AWC) dhidi ya Zambia.
Kikosi hicho chini ya Kocha Rogasian Kaijage kimepiga kambi katika hosteli ya Msimbazi Center kikiwa na wachezaji 25 kutoka 30 ambao kilianza nao katika kambi ya Mlandizi mkoani Pwani.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza dhidi ya Zambia itachezwa Februari 14 kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka. Timu zitarudiana wiki mbili baadaye jijini Dar es Salaam.
Wachezaji waliopo katika kikosi hicho ni Amina Ally, Amisa Athuman, Anastasia Anthony, Asha Rashid, Esther Chabruma, Eto Mlenzi, Evelyn Sekikubo, Fatuma Bashiri, Fatuma Hassan, Fatuma Issa, Fatuma Mustafa na Fatuma Omari.
Wengine ni Flora Kayanda, Happiness Hezron, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Najiat Abbas, Pulkeria Charaji, Shelder Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa, Winfrida Daniel na Zena Khamis.  
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top