********
WAZIRI wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper, amejiuzulu baada ya
kugundulika kuwa amemuajiri mfanyakazi asiyekuwa na kibali cha kufanya
kazi Uingereza.Harper ameeleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri mwaka 2007 kusafisha nyumba yake.
Bwana Harper ambaye amekuwa Waziri wa Uhamiaji tangu mwaka 2012, alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine na amemuomba radhi Waziri Mkuu, David Cameron kwa tukio hilo.
Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza.
Post a Comment