Taarifa
rasmi imetolewa na Chama cha Soka cha Misri kuwa mchezo wa marudiano
baina ya wenyeji Al-Ahly na Yanga, unaotarajiwa kupigwa Machi 9, mwaka
huu nchini Misri utachezwa bila kushuhudiwa na mashabiki.
Aidha
imeelezwa kuwa uamuzi huo umetokana na suala zima la kuimarisha ulinzi
kwa maofisa usalama na hasa ukizingatia mchezo wenyewe utachezwa majira
ya usiku. Timu ya Yanga inatarajia kuondoka nchi kesho usiku kuelekea
Misri kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo wa marudiano.
Post a Comment