Wakati Bunge maalumu la katiba likisubiri kupokea rasimu ya pili ya
katiba ili lianze mjadala, baadhi ya wasomi, wanaharakati na wananchi
wameonyesha wasiwasi wao juu ya weledi wa bunge hilo kutokana na masuala
mbalimbali yanayoendelea huko mjini Dodoma.
Wasiwasi huo unatokana na Wajumbe wa Bunge hilo kuendelea kuahirisha vikao na kuzozana kila mara hata katika masuala ya msingi yanayopewa kipaumbele yanayotakiwa kujadiliwa, tangu kuanza kukutana kwake tarehe 18 mwezi februari mwaka huu wakisema mengi ni masuala binafsi na misimamo ya itikadi za vyama.
Kwanza lilikuwa suala la nyongeza ya posho kutoka laki tatu zinazotolewa, kisha ukafuata mgawanyiko wa namna ya kupiga kura. Baadhi ya wananchi wanaona kuwa kinachoendelea mjini Dodoma hakitaweza kuwafikisha katika ndoto zao.
Baadhi wanahoji nguvu ya wajumbe 201 ambao wanatokea katika taasisi mbalimbali.

Wanadhani kuwa kundi hilo limedorora ndiyo maana wajumbe kutoka vyama
vya siasa wanalitawala bunge hilo.
Na ushiriki wa wanawake 100
walioteuliwa na Rais kuingia katika chombo hicho unazungumziwa pia.
Kuibuka kwa hoja mbalimbali ambazo baadhi zinalazimika kuundiwa kamati kunawafanya wananchi wapatwe na wasiwasi kuwa huenda mchakato huo ukachukua muda mrefu zaidi ya ule uliopangwa.

Rasimu ya pili ya katiba ambayo ndiyo itakayokuwa mjadala mkuu wa vikao vya bunge maalumu la katiba imekuja na mapendekezo mbalimbali ambayo yanawafanya wajumbe kuvutana juu ya uamuzi wake. Mojawapo ni suala la muundo wa serikali uliozifunika hata baadhi ya hoja zingine za msingi katika rasimu hiyo kama vile tunu za taifa na maadili ya viongozi.
Post a Comment