
Msemaji wa masuala ya usalama wa safari za ndege Australia, John Young, akiongea na waandishi wa habari.
Mabaki
ya ndege pichani ambayo kimoja kina ukubwa wa mita 24, yameonekana
umbali wa kilomita 2500 kusini Magharibi mwa pwani ya Australia.
Waziri mkuu wa Australia amesema kuwa
mitambo ya satelite ya nchi hiyo imenasa picha za vitu vinavyoonekana
kama mabaki ambavyo huenda ni ya ndege ya Malaysia iliyopotea siku 13
zilizopita.
Waziri mkuu huyo, Tony Abbott,
ameliambia bunge mjini Canberra kwamba picha za satelite zimeonyesha
vitu viwili vinavyofanana na mabaki ya ndege hiyo.
Taarifa hii imejitokeza karibu wiki
mbili baada ya ndege hiyo kutoweka na abiria zaidi ya 200 ikitokea mjini
Kuala Lumpur Malaysia kuelekea Beijing.
Msemaji wa masuala ya usalama wa safari
za ndege, John Young, baadaye alisema kuwa vitu hivyo ambavyo kimoja
kina ukubwa wa mita 24, vimeonekana umbali wa kilomita 2500 kusini
Magharibi mwa pwani ya Australia.
Aliongeza kwamba, hata hivyo, huenda vitu hivyo si mabaki ya ndege hiyo.
Wakati taarifa hii ilipotolewa, kulikuwa
na ndege ya Australia katika neo hilo , ndege zaidi zinatarajiwa
kuwasili katika eneo lenyewe na pia manowari ya jeshi inaelekea huko.
CHANZO: BBC SWAHILI



Post a Comment