
Picha za kinachodhaniwa kuwa mabaki ya ndege ya Malaysia nchini Australia
Ndege
na meli kutoka nchi mbali mbali zinaendelea kuitafuta mabaki ambayo
huenda yanatokana na ndege ya Malaysia iliyopotea takriban wiki mbili
zilizopita ikiwa imebeba takriban watu 240.
Matumaini
ya kutatua kitendawili hicho yaliongezeka baada ya Australia kutoa
picha za Satelaiti za vitu viwili vilivyoonekana baharini vuikidhaniwa
kuwa vifusi vya ndege hiyo.
Hata hivyo hadi kufikia sasa hakuna cha maana kilichopatikana.
Afisa mmoja mkuu wa New Zealand amesema operesheni hiyo ilitatizwa na kuchafuka kwa bahari na kutoona vizuri.
Meli ya mizigo ya Norway ilitumia taa kuyatafuta mabaki hayo pasina kufanikiwa.


Post a Comment