Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MCHEZAJI WA MANCHESTER UNITED ATANGAZA KUTANDIKA DARUGA.

 



Mchezaji raia wa Argentina na beki wa zamani wa klabu ya Man United Gabriel Heinze ametangaza kuachana rasmi na soka la ushindani kufuatia majeruhi ya mara kwa mara.Beki huyo ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Newell's Old boys amesema kila kitu katika maisha  kina mwisho wake.
Heinze akiongea hayo kupitia mtandao rasmi wa klabu yake alisema kuwa sehemu ya kikosi cha klabu nzuri ya kiargentina itabaki kuwa kumbukumbu muhimu kwa maisha yake,


"Nataka kusema kwamba mwisho wa msimu huu sitoweza kuendelea kuichezea tena klabu hii,siwezi kupambana tena na maumivu yangu na ninafahamu siwezi kushinda hii vita dhidi ya majeruhi,nilipenda kucheza hadi mwisho wa uhai wangu,lakini nafahamu siwezi kuwa mbinafsi."Gabriel Heinze

Heinze alianzia maisha yake ya soka katika klabu ya Newell's Old ya  nchini Aegentina kabla hajatimkia Vallodolid,PSG,Man United,Real Madrid,Marseille na Roma.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top