Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kata ya Nzi akijitambulisha Rasmi kwa Wananchi wa Kijiji cha Nzi kuwa yeye
ameamua kuachana na Chadema na Kujiunga na
CCM kwa hiari yake baada ya kupima Uwezo wa Chadema na CCM kwenye Hoja
na Matendo.Mwanachama huyu Mpya wa CCM ameahidi kuongoza timu ya Ushindi
kwenye Kata ya Nzi kuhakikisha Godfrey Mgimwa napita kuwa Mbunge.
Pia amesema ataiweka wazi mipango ya
Chadema na Watu wageni wa Chadema waliokodishwa na Kupangishwa Nyumba
kata ya Nzi wanaotembea Usiku kwaajili ya Kutafuta kura na kushambulia
Waoaunga mkono CCM kwenye kata ya Nzi.
Aliyekuwa
Mwanachama wa Chadema kutoka kijiji cha Kamiyu na Katibu Mwenezi wa
Chadema kata ya Kamiyu akitangaza kuachana na Chadema na Kujiunga na CCM
hii leo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Nzi.
Post a Comment