Staa
wa filamu Yobunesh Yusuph ‘Batuli’ amedaiwa kujiweka kwa Pedeshee Chifu
Kiumbe baada ya siku kadhaa zilizopita kumfuata na kumtaka amsaidie
katika project ya filamu yake .
Staa wa filamu Yobunesh Yusuph ‘Batuli’.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, baada ya msanii huyo kupewa sapoti ikiwa ni
pamoja na gari la kushutia, mdada huyo amekuwa akijionesha kuwa pedeshee
huyo ni mtu wake.
“Alipopewa
sapoti hiyo akaona ndiyo ajiweke kabisa bila kujua kuwa Chifu Kiumbe
alikuwa akimsaidia tu na wala hakuwa na wazo la kumtaka,” alidai sosi
huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Baada
ya habari hizi kunaswa, mapaparazi wetu walimtafuta pedeshehe huyo
ambaye alisema: “Hata mimi nashangaa kusikia watu wakisema natoka na
yule dada, ukweli sijawahi kuwa mpenzi wake alikuja kuniomba msaada wa
project yake nikamsaidia hata gari nilimpatia lakini nimesikia eti
ananiita bebi kwenye mitandao ya kijamii, siyo kweli kabisa.”
Batuli.
Batuli
naye anasemaje? Huyu hapa: “Mh! Watu wananisema mengi sana, waache
waseme, mimi naongea na Chifu kawaida tu, hata jana nilimfuata anisaidie
kama wasanii wengine.


Post a Comment