Mjumbe
wa Bunge la Katiba, Mhe. Ezekiel Oluoch akiingia jana kwenye kikao
cha Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Mhe. Uluoch, ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa Chama cha Walimu (CWT), ni mmoja wa wachangia mada wakubwa aliyejipatia umaarufu mkubwa mjengoni.

Mjumbe
ambaye ni mwakilishi wa wakulima Mhe.Hamisi Damumbaya akichangia
pamoja na kuwataka UKAWA kurejea kwenye mchakato wa katiba mpya.
Amewasifu viongozi wa dini kwa kutumia mahubiri kuelimisha wananchi
kuhusu katiba wakati wa kipindi cha ibada za Pasaka nchini kote.

Mwenyekiti wa
Bunge Maalum la KAtiba Mhe.Samwel sitta akiliambia Bunge jana kuwa
pamoja na UKAWA kuondoka koramu ya wabunge walio ndani ya ukumbi
imetimia kwa hiyo mchakato wa katiba mpya utaendelea kama kawaida.
Hii
inafuatia kikundi kinachojiita umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)
kususia Bunge wiki iliyopita, na baada ya baadhi yao kurudi na kuendelea
na bunge kama kawaida.
Wanaoendelea
na bunge wengi ni kutoka kundi la wateule 201 na baadhi ya vyama vya
upinzani ambao mwanzo walionekana kuunga mkono UKAWA.
Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa
Photo Solutions Wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati.
Post a Comment