Alhamisi
ya wiki hii Kampuni ya magari ya Nissan imezindua gari jipya lenye uwezo
wakipekee kabisa wa kujisafisha lenyewe na kuondoa kabisa uchafu wa
aina yoyote ile kwenye gari hilo.
Watengenezaji hawa wa magari aina ya Nissan wamefanya majairibio kwenye
gari hili kwa kutumia rangi maalum ya magari inayojulikama kwa jina la
"Ultra-Ever Dry" ambayo ina ondoa uchafu kwenye gari na kufanya gari
kujisafisha lenyewe.
Kampuni ya nissan wametoa taarifa rasmi na kusema kuwa ....
"Kwa kujenga tabaka la kinga ya hewa kati ya rangi na mazingira, kwa
ufanisi kabisa inazuia maji na uchafu wa barabara, kuunda na kuacha
alama chafu juu ya rangi ya gari, " Nissan walisema katika taarifa yao
Nissan wamesema kuwa Rangi hii inayo zuia uchafu kwenye gari, kwa hivi
sasa imefanyiwa majaribio kwenye gari aina ya Nissan Note na imeonyesha
mafanikio mazuri kabisa katika mazingira yote ikiwa ni katika sehemu
zenye hali ya hewa ya kawaida, sehemu zenye barafu, pamoja na sehemu
zenye maji maji.



Post a Comment