Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BURIANI GURUMO MUASISI WA MITINDO YA MSONDO, SIKINDE NA NDEKULE

                                      


 
gurumo_1_de4e5.jpg
Muhidin Maalim Mohammed Gurumo enzi ya uhai wake akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete.
********
Na Daniel Mbega
HABARI za kifo cha gwiji wa muziki nchini, Muhidini Maalim Mohammed Gurumo, zimeutikisa ulimwengu wa muziki. Tunaambiwa amefariki leo Jumapili Aprili 13 saa 9.00 alasiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kusumbuliwa na tatizo la mapafu kwa muda mrefu.
Miaka takriban minne iliyopita aliwahi kuzidiwa na kulazwa katika Hospitali ya taifa Muhimbili, na walilazwa pamoja na nguli mwingine wa muziki, Ramazan Mtoro Ongalla, maarufu Dk. Remmy Ongalla, ambaye jitihada za kupigania uhai hazikuweza kuishinda nia na mipango ya Mwenyezi Mungu. Akatangulia mbele ya haki.

Kifo ni wajibu wetu, kwa maana ndiyo maagizo ya Mungu baada ya baba yetu Adam na mkewe Hawa kutenda dhambi kule bustanini Aden.
Sote, ama wengi wetu, tunautambua mchango mkubwa kabisa wa Gurumo katika maendeleo ya muziki waTanzania. Kama Wazaire walivyokuwa wakimuenzi Verkys Kiamwangana Mateta, ndivyo ambavyo nasi tunastahili kuuenzi mchango wa Mjomba Gurumo.
Wapo wanamuziki wengi waliotangulia, wakatamba na bendi mbalimbali kama akina Salim Abdallah Yazidu na Ahmed Kipande, au akina Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, Marijani Rajabu Marijani, Hemedi Maneti Ulaya, na wengineo wengi, lakini kwa uhalisia, mchango wao hauwezi kufananishwa na huu wa Mjomba Gurumo.
Ndiyo. Wengine watamtaja 'Teacher' King Michael Enock Chinkumba aliyeziongoza Dar Jazz, Dar International na Sikinde, lakini bado tunaweza kusema mchango wa Gurumo ni kipekee katika maendeleo ya muziki wa dansi Tanzania. Amefanya makubwa sana kwa miaka 53 aliyodumu kwenye muziki.
Katika umri wake wa miaka 74, hakuna kazi nyingine yoyote aliyoifanya kwa mapenzi makubwa kama muziki. Sidhani na sina uhakika kama alikuwa mfanyabiashara ama mkulima.
Katika bendi zote tatu maarufu alizopitia, NUTA Jazz (zamani ikijulikana kama Kilimanjaro Chacha Band), Mlimani Park Orchestra na International Orchestra Safari Sound ya Hugo Kisima, alikuwa kiongozi, mwalimu, mtunzi na mwimbaji mahiri sana.
Mitindo aliyoibuni kwenye bendi hizo Msondo wa NUTA Jazz (baadaye ikaitwa JUWATA na OTTU), Sikinde wa DDC Mlimani Park na ule wa Ndekule katika IOSS ambayo haipo kwenye ramani ya muziki, ilishika hatamu nab ado inaendelea kutumika mpaka sasa huku Msondo ukibeba jina la bendi. Mitindo yote hiyo mitatu ni ngoma za Kabila la Wazaramo wanaopatikana mkoani Pwani.
Alizaliwa mwaka 1940 katika Kijiji cha Masaki wilayani Kisarawe katika Mkoa wa Pwani. Kutoka Masaki hadi Mzenga alikotokea Mbaraka Mwinshehe siyo umbali mrefu wa kutisha, hiyo ikimaanisha kwamba Pwani inajivunia historia ya wanamuziki wengi kuwahi kutokea huko wakiwemo Francis Lubua (Nassir Lubua) aliyekuwa anatokea Chalinze na Athumani Momba ambaye alikuwa anatokea maeneo ya Msanga wilayani Kisarawe.
Wakati fulani katika mahojiano enzi ya uhai wake aliweka bayana kwamba muziki ulikuwa kwenye damu yake tangu akiwa mdogo. Alirithi kwa mama yake ambaye alikuwa mahiri katika uimbaji wa ngoma ya Ndekule.
Alipopelekwa Dar es Salaam kwa mjomba wake Suleiman Sultan Mikole ikabidi wampeleke madrasa ili kupata elimu ya dini yake ya Kiislamu. Huku ndiko akaanza kujifunza kuimba kaswida.
Isome zaidi: BURIANI GURUMO MUASISI WA MITINDO YA MSONDO, SIKINDE NA NDEKULE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top