UVUMILIVU
umemshinda mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Javier Harnandez
`Chicharito` na sasa ameitaka klabu yake kumuuza majira ya kiangazi
mwaka huu baada ya kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.
Chicharito
ameongea mara tatu na bosi wake David Moyes katika miezi miwili
iliyopita juu ya yeye kunyimwa nafasi ya kucheza, huku akianzishwa
katika mechi tano tu za ligi kuu msimu huu.
Nyota
huyo raia wa Mexico ameiambia klabu yake kuwa atasikiliza ofa
zikazokuja juu yake majira ya joto na hadhani kama yupo katika mipango
ya Moyes hapo baadaye.
Chicharito ameshindwa kupata namba ya kudumu mbele ya Wayne Mark Rooney, Robin Van Persie na Danny Welbeck.
Sasa
mshambuliaji huyo amefikia maamuzi ya kuondoka huku akihusishwa na
mpango wa kuhamia Atletico Madrid kama mrithi wa Diego Costa mwenye kila
dalili ya kujiunga na Chelsea majira ya kiangazi.
Chicharito
mwenye miaka 25 alihuzunishwa baada ya kukosa nafasi ya kuanza kwenye
mechi ya robo fainali ya UEFA dhidi ya Bayern Munich, huku kocha Moyes
akimuanzisha Rooney ambaye hakuwa fiti kwa mechi ile.
Siku
nne Kabla ya kuwakabili Bayern, Chicharito alicheza dakika 90 katika
mechi ya ligi kuu dhidi ya Newcastle ambapo walishinda 4-0, hivyo
alijiona kuwa anastahili kuanza katika kikosi cha Man United kwa
kuzingatia kiwango chake kwenye mechi ile na mazoezi ya kujiandaa na
safari ya Allianz Arena.
Msimu
huu, mshambuliaji huyu amecheza mechi 31 katika mashindano yote, na
ameanzia benchi kwenye mechi 20, huku akifunga mabao 9 katika msimu huu
mgumu kwa David Moyes.
Nahodha
wa Man United, Nemanja Vidic naye yuko mbioni kujiunga na Inter Milan,
wakati huo huo Rio Ferdinand, Patrice Evra, Shinji Kagawa, Nani,
Anderson na Alex Buttner ni miongoni mwa wachezaji wengi wanaotarajiwa
kuondoka Old Traffo
Post a Comment