HIVI NDIVYO MLANGO WA OFISI YA MTENDAJI WA KATA YA MWENDAKULIMA ULIVYOFUNGWA NA DIWANI HUYO.
MWONEKANO WA OFISI ZA KATA YA MWENDAKULIMA ZILIZOJENGWA KWA UFADHILI WA MGODI WA BARRICK
MKUU WA WILAYA YA KAHAMA BENSON MPESYA MWENYE SHATI JEUPE AKIWASILI ENEO LA TUKIO.
MKUU WA WILAYA AKIENDA KUSHUHUDIA JINSI MLANGO HUO ULIVYOFUNGWA.
MTENDAJI WA KATA YA MWENDAKULIMA CESILIA CLEMENT AKIONYESHA JINSI DIRISHA LILIVYOVUNJWA NA WATU HAO.
MKUU WA WILAYA AKIWA KWENYE MLANGO HUO AKIANGALIA JINSI ULIVYOFUNGWA KWA BATI.
MKUU WA WILAYA AKIWA AMESIMAMA PEMBENI AKISHUHUDIA FUNDI AKIFUNGUA OFISI HIYO.
FUNDI AKIENDELEA NA KAZI YA KUFUNGUA AMLANGO HUO.
ASKARI AKIWA AMEBEBA JIWE NA BATI HILO BAADA YA KUFUNGULIWA ILI KUVIPELEKA KITUO CHA POLISI KWA AJILI YA USHAHIDI.
MSAFARA WA MKUU WA WILAYA UKIINGIA NDANI YA OFISI BAADA YA MLANGO KUFUNGULIWA.
MKUU WA WILAYA AKIWA NDANI YA OFISI HIZO.
MKUU WA WILAYA AKISAINI KITABU CHA WAGENI
MAKAMANDA WA SUNGUSUNGU WA KATA YA MWENDAJULIMA.
HAMISI ABBAS AMBAYE NI FUNDI SEREMALA ANAYETUHUMIWA KUSHIRIKIANA NA DIWANI HUYO KUFUNGA MLANGO HUO AKIWA CHINI YA ULINZI.
MTUHUMIWA WA PILI MAKAKA BENEDICTO AKIWA CHINI YA ULINZI.
DIWANI WA KATA YA MWENDAKULIMA NTABO MAJHABI AKIWA CHINI YA ULINZI KATIKA KITUO CHA POLISI KAHAMA.
Watu
wawili akiwemo na Diwani wa kata ya mwendakulima wilayani kahama mkoani
shinyanga Ntabo Majhabi jana wamekamatwa na jeshi la polisi akituhumiwa
kufunga ofisi za serikali za mtendaji wa kata hiyo.
Tukio
hilo limetokea jana majira ya saa tano asubuhi baada ya mtendaji wa
kata hiyo Cesilia Clement kupigiwa simu na mlinzi wa ofisi hizo Joseph
Katambi na kumpa taarifa za tukio hilo liliofanywa na wananchi 15
walioambatana na diwani huyo.
Kwa
mujibu wa mtendaji wa kata hiyo Cesilia Clement amesema kuwa waliamua
kuibadirisha kamati ya sungusungu ya kata hiyo hali ambayo ilianza
kuleta malalamiko na minong’ono ya chini kwa chini jambo lililoonyesha
kuwa kuna watu walikuwa na maslahi na kamati hiyo.
Cesilia ameongeza kuwataja wengine waliokamatwa katika tukio hilo ni pamoja na Hamisi Abbas ambaye ni Fundi selemala na Makaka Benedicto wote wakaazi wa kata hiyo.
Kufuatia
hali hiyo mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akiongozana na kamati
ya ulinzi ya kata na askari polisi walifika katika ofisi hiyo na
kushuhudia jinsi mlango huo ulivyofungwa kwa kuwekewa kipande cha bati
na kupigiliwa misumari tisa pamoja na mawe.
Aidhaa
mkuu huyo wa wilaya alitoa amri ya kuvunjwa kwa bati hilo chini ya
ulinzi wa askari polisi na kuamrisha wahusika wote waliofanya tukio hilo
la kufunga ofisi za serikali ambazo zinahudumia wananchi kukamatwa
akiwemo diwani wa kata hiyo.
Mpesya
ameongeza kuwa kitendo hicho ni fedheha na kwamba ni jambo lisiloweza
kuvumilika na kwamba ikiwa wamefunga ofisi ya mtendaji ipo siku
watafunga ofisi ya mkuu wa wilaya kama sheria haitochukua mkondo wake.
Kwa
upande wake mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa kata hiyo Cesilia
Makula amesema kuwa kitendo hicho ni njama ambazo watu hawazijui na
kwamba diwani huyo angetakiwa kufikisha malalamiko hayo ofisi ya
mkurugenzi na siyo kuchukua maamuzi ya kufunga ofisi ya serikali.
Makula
ameongeza kuwa watu hao waliofanya tukio hilo walikusanywa na diwani
huyo kwa pikipiki na kwamba aliwaita waandishi wa habari ili kutoa
taarifa hizo za kuifunga ofisi hiyo.
DIWANI MAJABI AKIONGOZA ZOEZI LA KUUFNGA OFISI HIYO SIKU YA TUKIO |
Awali
Katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Mwendakulima
Diwani huyo akiwa anawahutubia wananchi alimtuhumu Mtendaji huyo
kujihusisha na hujuma za ajira katika mgodi wa Buzwagi ambazo hupitia
kwenye ofisi yake.
Aidha
amesema tuhuma zingine ni kuwaweka mahabusu wananchi wanaodai haki ya
kusomewa mapato na matumizi ya michango yao hali ambayo Diwani huyo
aliwataka wananchi wamuunge mkono kuifunga ofisi ili aondoke kufanya
kazi kwenye eneo hilo.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka jeshi la Polisi wilayani Kahama Diwani huyo
na wenzake wawili wanatarajia kufikishwa mahakamani siku ya jumatatu
kujibu tuhuma hizo zinazowakabili.
CHANZO:DUNIA KIGANJANI
Post a Comment