H.baba kutoka wikiendi iliyopita amefanya ziara
ya kutembelea familia ya James Dandu ambayo iko Mwanza ambapo pia
alifika mpaka lilipo kaburi lake Ngudu,Kwimba hapo H.baba alipalilia
pamoja na kutoa heshima zake kwenye kaburi la Muasisi huyu wa tuzo za
Tanzania.
Mbali na kuwa muasisi tu Cool James ambaye alifariki Agost 2002
alikua ni miongoni mwa wasanii wa kwanza kuutangaza muziki wa Bongo
Fleva nje ya nchi,Hizi ni picha baadhi ambazo zinamuonyesha H.baba akiwa
na familia pamoja kaburi alilozikwa James Dandu.
H. Baba akiwa na wazazi wa marehemu Cool James
H baba akifanya usafi kwenye kaburi la Dandu. Chanzo:bongo5
Post a Comment