Wajumbe wa Bunge la Katiba wakiwa bungeni mjini Dodoma jana.Picha na Emmanuel Herman
 
Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma ni vituko, vioja, uchafuzi, lugha za matusi, mipasho kama ‘kitchen party’ au uwanja wa fisi pale kwenye bar ya rafiki yangu wa kitambo mwandishi mwezangu Baraka Karashani.
Kwani wajumbe wa Bunge la Katiba hawana aibu, woga au ndiyo kusema mshipa wa aibu umeingia mafuta ya taa waheshimiwa nyie kulikoni jamani mbona taabu wananchi hawaelewi nini kinaendelea maana ni serikali tatu au mbili kama msahafu vile ahhaaaaa jamani.

Kwa sababu watu wazima kurushiana matusi kama vile mpo kwenye gurio la nguo au mnandani au sewa kwa madada zetu pale Buguruni haileti picha kwa wananchi wanaotizama Bunge hilo nchi nzima halafu mnachukua 300,000 kwa siku kibindoni kwenye nyama choma chako chako maana yake nini?
Kwa mantiki hiyo basi jana nilitamani kwa udi na uvumba kutizama angalau kwa masaa kadhaa majadiliano ya Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kwa kutambua umuhimu wake kwa vizazi vya sasa na vijavyo kwa hiyo niliamua kwa makusudi kabisa kutizama wajumbe wa Bunge hilo maalum wakirubana kwa hoja na si kwa vioja.
Lakini Mjumbe pekee aliyenikuna jana ni Mhe Mbarouk Salum Ally kutoka visiwani aliyesema kwamba wajumbe kutoka Zanzibar wamekuwa kama “Mbayuwayu’ vigeugeu kwa sababu wakiwa visiwani wanataka serikali tatu kwamba muungano unawabana wakija Dodoma wanalowa maji wapole kama maji ya mtungi hivi ni kweli?
Eti ni kwanini wazanzibari wanalalamika kuhusu kero za muungano kila kukicha mara hili mara lile lakini wakipata fursa wanaufyata kama alivyosema Jussa juzi au si kweli jamani nini kinatokea mpaka wakifika Dodoma hoja zao zinakuwa kapuni kabisa!
Mjumbe huyo wa Bunge la katiba amesema kwamba wazanzibar wengi ndani ya Bunge na hasa wa kutoka chama tawala wanalalamika chini kwa chini na wakiwa visiwani wanasema sasa tunataka serikali tatu yaani serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Shirikisho lakini wakifika kwenye vikao vya chama chao wanaloa kabisa hawathubutu kabisa kusema chochote!
Lakini hebu tujikumbushe kidogo wazanzibari kulalamika kwamba serikali ya bara inawabana au Tanganyika kujificha ndani ya Muungano haikuanza leo yaani piga ua huo ndio ukweli malalamiko ya watu wa visiwani kuhusu muundo wa muungano yalianza tangu mzee karume watu wanasema na baadaye Aboud Jumbe ambaye alitiwa ndani kabisa kwa kile wanachosema watu kuchafuka kwa hali ya hewa 1984.
Kwa hiyo swala la muundo na kero za muungano lipo kitambo Zanzibar inataka mamlaka yake kamili na ndiyo maana hivi karibuni 2010 waliandika katiba yao na kutamka bayana kwamba Zanzibar ni nchi ndiyo ambayo kimsingi inasigana na katiba ya Muungano nani anabisha?
Sasa kinachofanya wasiseme ukweli kwamba jamani serikali tatu ndio suluhisho la kudumu la kero za muungano ni kipi? Basi kuanzia sasa kama hawawezi na tumpe rungu Jakaya kikwete ya kuwalazimisha kubadili katiba yao na Zanzibar si nchi tena mbali ni sehemu ya Muungano ndiyo kwa hapo nami namuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kwa hilo.
Hata kama rasimu ya katiba ya Jaji warioba inasema serikali tatu ndio maoni ya wananchi lakini kwa sababu wenyewe Zanzibar wameridhika na muundo wa sasa hakuna shida kazi ni moja kwa chama tawala kuhakikisha Rais wa SMZ Ali Mohammed Shein anabadilisha vipengele kadhaa kwenye katiba yao ya 2010 ili twende sawa ndiyo.
Watasema sana lakini huo ndiyo ukweli waache malumbano yasiyokwisha huko mjengoni kama vilabu vya pombe ya kibuku na mnazi kama uwanja wa fisi!
Naomba kuwasilisha 
 
credit: Mhariri Mkuu MOblog Tanzania