Licha
ya madudu yanayofanywa na baadhi ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba
wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Katibu Mkuu CCM,
Abdulrahman Kinana amewata Watanzania kuwa watulivu akisema ni lazima
Katiba mpya itapatikana huku akisisitiza watambue kuwa Katiba hiyo si
mwarobaini wa matatizo yaliyopo sasa hapa nchini. Kiongozi huyo
akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapa ikiwa ni
hitimisho la ziara yake ya siku 20 katika mikoa minne, Dar es salaam
,Rukw, Kigoma na Katavi ya kukagua utekelezaji wa ilani na kuimarisha
chama hicho. Katika mkutano alikuwa akizungumzia matukio yanayoendelea
kutokea Bunge la Katiba ambapo aliwatoa hofu Watanzania kuwa hayazuii
kupatikana kwa Katiba hiyo kama iliyopangwa.Akitolea mfano nchi
ambazo zina Katiba bora duniani kama
vile Afrika Kusini na Namibia ambazo hadi leo bado maisha ya wananchi
wake yako vilevile kwa kuwa utekelezaji wa mwongozo huo unakwenda hatua
kwa hatua. Alisema kinachoendelea kwa sasa bungeni ni wazi baadhi ya
watu kutoka vyama vya upinzani akili zao zimejikita katika uroho wa
madaraka na ndio maana wanang’ang’ania mfumo wa Serikali tatu wakiwa na
imani kuwa huenda wakapata madaraka. Alibainisha kuwa chama hicho
kimekuwa kikalaumiwa kuwa kinatawala maamuzi ya Bunge kutokana na wingi
wa wabunge wake, jambo ambalo alikiri na kusisitiza kuwa wabunge hao
hawakujipeleka wenyewe kwenye Bunge bali walichaguliwa na wananchi na
maamuzi wanayotoa yanatokana na wananchi. Naye Katibu wa Halmashauri Kuu
ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema yanayoendelea
bungeni kwa sasa yasiwasumbue akili wananchi kwa kuwa chama hicho
kitahakikisha Katiba mpya yenye mtazamo na matakwa ya wananchi
inapatikana. Alisema kitendo cha utawla kuanzisha migogoro na kutoka nje
ya Bunge ni kutafuta umaarufu kutokana na ukweli kuwa tayari
walishalipwa posho ya siku sita hivyo kutoka kwao kuwaathiri kimaslahi.
Alisema kitendo cha UKAWA kuanzisha migogoro na kutoka nje ya bUnge ni
kutafuta umaarufu kutokana na ukweli kuwa tayari walishalipwa posho ya
siku sita hivyo kutoka kwao hakuwaathiri kimaslahi.
on Sunday, April 20, 2014
Post a Comment